![Meet-A-Turtle-That-Smokes-10-Cigarettes-A-Day.jpg2](http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/08/Meet-A-Turtle-That-Smokes-10-Cigarettes-A-Day.jpg2_.jpg)
Maajabu hayaishi duniani na kila siku yanajitokeza maajabu mapya ambayo hukuwahi kutarajia kuyashuhudia maishani mwako . Nchini Japan kuna kobe ambaye amejiingiza kwenye tabia ya uvutaji wa sigara na mpaka sasa anavuta sigara kumi kwa siku.
Kobe huyu alianza tabia ya kuvuta sigara wakati mmiliki wake Bwana Tang alipojaribu kuutoa mfupa wa kuku uliokuwa umekwama tumboni mwa kobe huyo .
Kobe
alimg’ata wakati jamaa alipojaribu kuingiza mkono wake kinywani mwa
kobe , Mr Tang aliamua kuiweka sigara aliokuwa akiivuta yeye mwenyewe
mdomoni mwa kobe ili kumziba asimng’ate tena . Kobe aliivuta sigara ile
huku akiutoa moshi mdomoni kama kawaida na ndani ya dakika tatu ilikuwa
imeisha na mpaka sasa imekuwa
tabia na kobe huyo anavuta mpaka sigara kumi kwa siku moja . Mr Tang
anatafuta njia ya kumuachisha kobe tabia hiyo ya uvutaji sigara.
No comments:
Post a Comment