Robert Lewandowski amepiga Bao 3 wakati Borussia Dortmund ilipotoka nyuma na kuibamizaStuttgart Bao 6-1 na kutua kileleni mwa Bundesliga.
Karim Haggui aliifungia Stuttgart Bao
lao mapema lakini Sokratis Papastathopoulos akasawazisha kwa kichwa na
Marco Reus kufunga Bao la pili kwa Dortmund.
Ndipo zikaja Bao 3 za Lewandowski na Pierre-Emerick Aubameyang kumalizia Bao la 6.
MAGOLI:
Borussia Dortmund 6
Papastathopoulos Dakika ya 19
-Reus 22
-Lewandowski 54,, 56 & 72
-Aubameyang 81
VfB Stuttgart 1
-Haggui 13′
Tayari Msimu huu Lewandowski amepiga Bao
12 katika Mechi 14 na kuifanya Dortmund iongoze Bundesliga ikiwa Pointi
2 mbele ya Bayern Munich ambao wana Mechi moja mkononi na wanacheza
Ugenini na Hoffenheim Siku ya Jumamosi.
Dortmund sasa wanaingoja Arsenal itembelee Signal Iduna Park hapo Jumatano kwa Mechi ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Katika Mechi ya Kwanza ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI iliyochezwa Mwezi Oktoba, Arsenal, wakiwa kwao Emirates, walilala
Bao 2-1 na Borussia Dortmund.
No comments:
Post a Comment