Saturday, 9 November 2013

MOURINHO ALIA NA RATIBA LIGI KUU ENGLAND

MOURINHO-CHELSEA_TRAINING

 MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amedai Watu ambao wanatengeneza Ratiba ya Ligi Kuu England wanaicheka Timu yake.
Akiongelea kuhusu Mechi yao ya Ligi ya Jumamosi na West Bromwich Albion, Mourinho amelalamika kuwa kupewa Siku 3 toka Mechi yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Schalke waliyocheza Jumatano na kucheza tena Jumamosi wakati Klabu za Jiji la Manchester, Man United na Man City, na Arsenal zina Siku 4 toka Mechi zao za Ulaya sio sawa.

Mourinho anaamini Chelsea Msimu huu hawakutendewa haki mara kadhaa kwenye upangaji Ratiba.
Amesema: “Nahisi Mechi yetu Wikiendi hii ni spesho kwa sababu Timu zote za England zilizocheza Ulaya, hasa zile za UEFA CHAMPIONZ LIGI, sisi ndio Timu pekee tunacheza Jumamosi. Kila Mtu ana Siku moja ya nyongeza ya kupumzika ila sie tu ambao tunacheza Jumatano na Jumamosi. Wengine Jumanne na Jumapili. ”
Ameongeza: “Hili linatokea mara nyingi. Tulicheza na Arsenal hivi hivi na sasa inabidi tucheze tena. Nadhani wanacheka. Wanajua nini wanaweza kufaya na kucheka wakijua siwezi kufanya lolote.’

LIGI KUU ENGLAND  WIKI END HII
    
RATIBA

Jumamosi Novemba 9
18:00 Aston Villa v Cardiff
18:00 Chelsea v West Brom
18:00 Crystal Palace v Everton
18:00 Liverpool v Fulham
18:00 Southampton v Hull
20:30 Norwich v West Ham
Jumapili Novemba 10
15:00 Tottenham v Newcastle
17:05 Sunderland v Man City
19:10 Man United v Arsenal
19:10 Swansea v Stoke

No comments:

Post a Comment