Monday, 30 September 2013

PICHA ZA JK ALIPOTUA DAR ES SALAAM HAPO JANA AKITOKEA CANADA NA MAREKANI...

00 3c708
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 wakitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
b3 dd083

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda huku Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali akiangalia wakati alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2013 akitokea Marekani katika ziara ya kikazi.

YANGA YAAMUA KUFANYA KWELI,WAITEKA JANGWANI: TAARIFA KUHUSU MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA UWANJA


fmk_e96ee.gif
LEO tungependa kupitia kwenu kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wetu wa Uwanja wa kisasa wa mpira katika Jiji la Jangwani kama itakavyojulikana
Mara ya mwisho tuliongea ama kuonana ilikuwa mwezi wa tatu wakati Ndugu zetu wa BCEG walipokabizi Concept design ama Usanifu wa awali na kuanzia sasa tutakuwa tunatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mradi huu. Wahenga walisema UKICHA KUSEMA HUTATENDA JAMBO lakini pia KUKAA KIMYA SANA kunajenga hisia mbaya na kutoa nafasi ya upotoshwaji wa habari.
Kwa kifupi napenda kuwakumbusha kuwa Makubalino ya Awali (Memorandum of Understanding) yalisainiwa 23 Novemba 2012. Pamoja na mengineyo YANGA inatakiwa:

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE OCTOBER 1

 

DSC 0051 4272d
DSC 0052 dc9bc
DSC 0053 c8425
DSC 0054 b1a66
DSC 0055 c8707
DSC 0056 eef90
DSC 0057 a289d
DSC 0058 4d696
DSC 0059 78ecb

LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA KUENDELEA WIKI HII KATIKA VIWANJA TOFAUTI KUFUKA NYASI.

                KESHO OCTOBER 01 2013
Zenit St PetersburgvFK Austria WienPetrovski Stadium

ArsenalvNapoliEmirates Stadium

BaselvFC Schalke 04St Jakob-Park

AjaxvMilanAmsterdam Arena

CelticvBarcelonaCeltic Park

FC PortovAtltico de MadridEstadio do Dragao

Borussia DortmundvMarseilleSignal Iduna Park

Steaua BucharestvChelseaStadionul Ghencea

    JUMATANO 02 October 2013
CSKA MoscowvViktoria PlzenArena Khimki

Paris Saint GermainvBenficaParc des Princes

RSC AnderlechtvOlympiakosConstant Vanden Stock

Manchester CityvFC Bayern MnchenEtihad Stadium

Shakhtar DonetskvManchester UnitedDonbass Arena

Bayer 04 LeverkusenvReal SociedadBayArena

JuventusvGalatasarayJuventus Stadium

Real MadridvFC KbenhavnSantiagoBernabu

AMRI KIEMBA WA SIMBA APATA UGONJWA KAMA UNAOMTESA MESSI BARCA


Missing: Messi is out for three weeks with a hamstring problem, picked up in Barcelona's win at AlmeriaKIUNGO tegemeo wa Simba SC, Amri Ramadhani Kiemba amepata ugonjwa sawa na ambao unamuweka nje Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi kwa wiki tatu, huo si mwingine ni maumivu ya nyama.
Tofauti tu ni kwamba, Muargentina wa Barcelona ya Hispania, Messi maumivu yake ni ya mguu wa kulia, wakati Kiemba ni mguu wa kushoto.
Kiemba aliumia jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC ikishinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lakini Kiemba aliyewahi kuchezea Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga SC ya Dar es Salaam na Miembeni ya Zanzibar alisema hatarajii kama maumivu yake yatamuweka nje muda mrefu kama Messi.
“Mimi sihisi maumivu sana, ni kidogo tu, ngoja nijisikilizie siku moja na pia nitasikiliza ushauri wa Daktari, baada ya hapo nitajua itakuwa ni muda gani,”alisema Kiemba jana baada ya kuulizwa kuhusu hali yake.
Simba SC ilipata pigo dakika ya 30 tu jana, baada ya kiungo wake huyo mwenye rasta na muumini safi wa dini ya Kiislamu, Kiemba kuumia na kutoka nje, nafasi yake ikichukuliwa na Ramadhani Singano ‘Messi’, aliyekwenda kufunga bao la pili. 
Atakosekana: Messi atakuwa nje kwa wiki tatu kutokana na maumivu ya nyama, aliyoyapata katika mechi kati ya Barcelona na Almeria 

Katika mchezo huo, hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Mrundi Amisi Tambwe dakika ya 24 kwa penalti, baada ya beki Jamal Said wa JKT Ruvu kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha pili, Simba SC walikianza kwa kasi na kufanikiwa bao la pili dakika nne tu tangu kuanza kwa ngwe hiyo ya lala salama kupitia kwa Messi wa Msimbazi.
Messi alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira uliorudishwa na mabeki wa Ruvu kufuatia Amisi Tambwe kuunganisha krosi maridadi ya Abdulhalim Humud ‘Gaucho’.
Kwa matokeo hayo, Simba SC inatimiza pointi 14 baada ya kucheza mechi sita na kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo.
Lionel Messi ataikosa mechi ya kesho ya Ligi ya Mabingwa Kundi H ugenini dhidi ya Celtic ya Scotland, na kuwa nje kwa wiki tatu nyingine, baada ya kuumia nyama za mguu wake wa kulia. 
Mwanasoka huyo bora wa dunia alitolewa wakati timu yake ikhinda 2-0 dhidi ya Almeria Jumamosi muda mfupi tu baada ya kufunga bao la kwanza dakika ya 21, ambalo lilikuwa bao lake la nane msimu huu.

Saturday, 28 September 2013

BARAZA LA USALAMA LAIDHINISHA AZIMIO KUHUSU SYRIA


  • syria_UN_fb37a.jpgBaraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio jana Ijumaa(27.09.2013)ambalo linataka kuondolewa kabisa kwa silaha za sumu nchini Syria lakini halitishii kuchukuliwa hatia za kuiadhibu serikali ya rais Bashar al-Assad iwapo haitatekeleza.
Kura hiyo ambayo imepigwa kwa kauli moja na wajumbe wote 15 wa baraza la usalama imefikisha kilele wiki kadha za majadiliano ya kidiplomasia kati ya Urusi na Marekani. Ilikuwa katika msingi wa makubaliano kati ya nchi hizo mbili yaliyofikiwa mjini Geneva mapema mwezi huu kufuatia shambulio la gesi ya sarin Agosti 21 mwaka huu katika kitongoji kimoja cha mji wa Damascus ambapo mamia ya watu wameuwawa.
Makubaliano ya Urusi na Marekani
Makubaliano kati ya Urusi na Marekani yameepusha hatua za kijeshi dhidi ya serikali ya Assad, ambapo serikali ya Marekani inaishutumu kwa shambulio la hapo Agosti. Serikali ya Syria na mshirika wake, Urusi , wanawalaumu waasi wanaopambana na serikali kwa shambulio hilo. Sehemu moja ya azimio hilo , lilielezewa na wanadiplomasia wa baraza hilo kuwa ni muhimu, linaidhinisha mpango kwa mpito wa kisiasa nchini Syria uliokubalika katika mkutano wa kimataifa mjini Geneva Juni mwaka 2012. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema baada ya kura hiyo kuwa mataifa makubwa yanamatumaini ya kufanya mkutano wa amani kwa ajili ya Syria katikati ya mwezi Novemba mjini Geneva.

RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA: LEO JUMAMOSI....MWALIMU KUKUTANA NA MWANAFUNZI WAKE


Barclays-Premier-League-fixtures-May-_05dde.jpg

14:45 Tottenham Hotspur na Chelsea
17:00 Aston Villa na Manchester City
17:00 Fulham na Cardiff City
17:00 Hull City na West Ham United
17:00 Manchester United na West Bromwich Albion
17:00 Southampton na Crystal Palace
19:30 Swansea City na Arsenal

Friday, 27 September 2013

Sheikh Sharrif Ahmed; Rais Anayedhibiti Maeneo Jirani Na Ikulu..


shehki_871e3.jpg
Ni Rais wa Somalia. Kwa hakika, kwa sasa ndiye Rais wa nchi ya Kiafrika mwenye wakati mgumu sana. Na katika shida zake, Sheikh Sharrif ameonekana, si mara moja, akitua Dar Es Salaam, kwenye Ikulu ya JK. Kwa Sheikh Sharrif aliye matatizoni, kufunga safari ya Dar kwa JK ni kama kwenda kwa Obama! Kuna tofauti kubwa na Mogadishu.
Kiukweli Sheikh Sharrif Ahmed hana eneo kubwa la nchi ambalo anaweza kusema kuwa analidhibiti. Kuna wakati ikasemwa, kuwa anadhibiti maeneo jirani tu na Ikulu yake ya Mogadishu. Huko kwengine kuna ' Mabwana wa Vita'.
Na sasa ni ' pasua' kichwa ya Al shabaab. Tofauti na inavyoonekana nje, Al shaabab hawajawa na nguvu za kutisha sana. Isipokuwa, wakiachwa wakue, ni ' pasua' kichwa si tu kwa Somalia, bali kwa nchi zetu hizi.(P.T)
Shambulizi la Wastgate ni ishara za Al Shabaab wanaoanza kuota mapembe. Kuna mantiki ya Marais wa nchi jirani na Somalia ikiwamo Tanzania, chini ya mwevuli wa AU na UN, kufanya jitihada za kuungana katika kupanga mikakati ya kumsaidia Sheikh Sharrif Ahmed.
Wamsaidie ili Somalia itawalike. Na kwa kufanya hivyo, kutaharakisha vita ya kuisambaratisha Al Shabaab, ambayo kimsingi, haina sapoti ya Wasomalia wengi.

LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA WIKI END HII, YANGA KUFUTA MACHUNGU NA RUVU??

Print PDF
>>VINARA SIMBA JUMAPILI NA JKT RUVU
>>AZAM, COASTAL WAGENI MBEYA!!
RATIBA
Jumamosi Septemba 28
Yanga v Ruvu Shooting
Rhino Rangers v Kagera Sugar
Mbeya City v Coastal Union
Mgambo JKT v JKT Oljoro
Jumapili Septemba 29
Ashanti United v Mtibwa Sugar
JKT Ruvu v Simba
Tanzania Prisons v Azam FC
++++++++++++++++++++++
VPL_2013-14_LOGO-NEWMabingwa Watetezi wa VPL, LIGI KUU VODACOM, Yanga, wanarejea tena kwenye Ligi wakitoka kwenye kipigo cha 3-2 walichokipata Jumapili iliyopita toka kwa Azam FC na Jumamosi wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Ruvu Shooting.
Kichapo hicho cha Azam FC kimeifanya Yanga ishike Nafasi ya 9 kwenye Ligi ikiwa na Pointi 6 kwa Mechi 5 baada kushinda Mechi moja, Sare 3 na Kufungwa moja huku wapinzani wao wa Jumamosi, Ruvu Shooting, wakiwa Nafasi ya 4 na wana Pointi 9 kwa Mechi 5.
Vinara wa Ligi hii, Simba, wenye Pointi 11, wao watacheza Jumapili na Ruvu JKT ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 9.
Timu za Azam FC na Coastal Union, ambazo pia zina Pointi 9 kama vile JKT Ruvu na Ruvu Shooting, zote zipo huko Mbeya ambapo Jumamosi Coastal Union wataivaa Mbeya City na Jumapili Tanzania Prisons wataikabili Azam FC.
VPL-MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
GF
POINTI
1
Simba SC
5
3
2
0
9
13
11
2
JKT Ruvu
5
3
0
2
4
6
9
3
Azam FC
5
2
3
0
3
8
9
4
Ruvu Shooting
5
3
0
2
3
6
9
5
Coastal Union
5
2
3
0
3
5
9
6
Kagera Sugar
5
2
2
1
3
6
8
7
Mbeya City
5
1
4
0
1
6
7
8
Rhino Rangers
6
1
4
1
0
7
7
9
Yanga SC
5
1
3
1
3
10
6
10
Mtibwa Sugar
5
1
3
1
-1
4
6
11
JKT Oljoro
5
1
1
3
-2
3
4
12
Mgambo JKT
5
1
1
3
-8
2
4
13
Prisons FC
5
0
3
2
-6
2
3
14
Ashanti United
6
0
1
5
-11
2
1

Kurasa za magazeti leo jumamosi september 28

 

DSC 0066 048af
DSC 0067 182bf
DSC 0068 b4d0a
DSC 0069 8f52d
DSC 0070 85aa4
DSC 0071 12cca
DSC 0072 73576
DSC 0073 9c3d8
DSC 0074 4e069
DSC 0075 986c5
DSC 0076 8b85b
DSC 0077 089bc

Kuhusu maziko ya Wanajeshi na huyu Mtangazaji waliouwawa kwenye shambulio la Westgate Kenya

36
Mwanajeshi wa kwanza alieuwawa
1. Isaya Kibet Terer ni mmoja wa Wanajeshi waliopoteza maisha kwenye harakati za kuokoa watu waliokua wametekwa kwenye jumba la kibiashara la Westgate Nairobi Kenya.
2. Ni Mwanajeshi aliekua na miaka miwili tu toka aingie jeshini, alikua anafanya biashara pia ambapo alikua na daraja la Uluteni jeshini na umri wake ulikua miaka 23 tu lakini pia alikua anategemewa kuisaidia familia yake.
3. Kingine kumuhusu Mwanajeshi huu ambae alikua miongoni mwa Wanajeshi 11 waliojeruhiwa kwenye harakati za uokoaji ni kwamba alikua afunge ndoa mwezi December mwaka huu.
Mwanajeshi wa pili aliyeuwawa:
Onyango Opodi ambae alikua Luteni ni miongoni mwa Wanajeshi waliouwawa kwenye uokoaji kwenye jumba la Westgate ambapo kifo chake kimetokea siku tatu tu baada ya Mwanajeshi huyu kurudi Kenya akitokea Somalia alikokua amejiunga na jeshi la Kenya kwenye Opareshen.
Ruhila 1Mtangazaji Ruhila Adatya:
Ni miongoni mwa waliofariki kwenye shambulio la Westgate ambapo alifariki dunia akiwa na ujauzito njiani akikimbizwa hospitali baada ya kupata majeraha yaliyotokana na shambulio la magaidi Westgate.
Adatya alikua akiandaa kipindi cha mapishi cha TV kilichokua kinafanyika kwenye jumba hilo la Westgate ambapo kilikua ni shindano la Watoto kushindana kupika.
Mmoja wa mashuhuda amesema mtangazaji huyu wa East FM, Kiss TV, X Fm, Kiss 100 na E News.

Wakuu wa usalama kuhojiwa Kenya




Sehemu ya jengo la Westgate iliyoporomoka
Maafisa wakuu wa ujasusi wametakiwa kufika mbele ya kamati ya ulinzi ya bunge ili kuhojiwa kuhusu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jumba la Westgate mjini Nairobi.
Taarifa kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaonyesha kuwa hali ya kulaumiana imeanza kuibuka huku mashirika ya usalama yakinyosheana kidole.
Watu 67 waliuawa kwenye shambulizi hilo huku zaidi ya miamoja sabini na tano wakipata majeraha mabaya. Shirika la Red Cross nalo linasema kuwa watu 61 wangali hawajulikani waliko.
Wataalamu wa uchunguzi wa mauaji wangali wanafanya uchunguzi wao wakitafuta miili na dalili za kilichosababisha shambulizi hilo.
Kamati ya bunge inataka maafisa wanaohusika na maswala ya usalama waweze kuwajibishwa.
Kundi la kigaidi la nchini Somalia, al-Shabab limedai kufanya mashambulizi hayo yaliyodumu siku nne kama hatua ya kulipiza kisasi kwa Kenya kujihusisha nchini Somalia kijeshi.
Hii leo ni siku ya tatu ya maombolezi kwa wathiriwa wa shambulizi hilo wakiwemo raia na wanajeshi.
Rais Uhuru Kenyatta amehudhuria mazishi ya mpwa wake na mchumba wake mjini Nairobi ambapo aliwahutubia waumini.

Walipuuza onyo?

Hatua ya kuwataka maafisa hao wa usalama kufika mbele ya tume ya bunge siku ya Jumatatu, inakuja kutokana na wasiwasi miongoni mwa wakenya kuhusu kiwango cha maafisa hao kujiandaa kwa tukio lolote la kigaidi sawa na lililotokea Westgate.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mmoja wa maafisa waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni mkuu wa shirika la ujasusi Michael Gichangi, anayesema alitoa taarifa za ujasusi kuhusu shambulizi hilo kwa polisi.
Lakini, afisaa mmoja mkuu katika idara ya polisi alikana kuwa taarifa hiyo ilitolewa kwa polisi.

MRISHO NGASSA: NAWALIPA SIMBA MWENYEWE NIRUDI KUITUMIKIA KLABU YANGU YA YANGA"


Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), Mrisho Ngassa ameamua kulipa mwenyewe deni lake la Sh45 milioni anazotakiwa kuilipa klabu ya Simba baada ya kuhukumiwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Awali Ngassa alikuwa ameweka ‘ngumu’ kulipa fedha hizo na kuzua tafrani kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kuhusiana na adhabu yake ya kulipa fidia iliyotolewa na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi ya Wachezaji ya TFF.
Kamati hiyo ilimfungia Ngassa kucheza mechi sita, adhabu ambayo amekwisha itumikia na kilichobakia sasa ni kulipa fedha hizo ili aweze kucheza mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Pamoja na Ngassa kuonyesha juhudi kubwa mazoezini, sakata la ulipaji wa fedha hizo lilizua tafrani nyingine huku uongozi ukitaka kulipa fedha hizo, lakini kwa masharti ya kuongeza mkataba mwingine.
Hali hiyo ilizua maswali mengi kutokana na ukweli kuwa muda wa kuingia mkataba kwa mujibu wa taratibu za TFF ulikuwa umekwisha na suala hilo lingeweza kufanikiwa wakati wa dirisha dogo la usajili.
Baada ya kukaa kimya cha muda mrefu, Ngassa ameamua kutangaza waziwazi kuwa atalipa fedha hizo  alizochukua kutoka Simba  na faini ambayo Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi ya Wachezaji iliyoamua. Kamati hiyo ilimtaka Ngassa kulipa fidia ya asilimia 50 ya fedha Sh30 milioni alizochukua kutoka Simba.
Ngassa alisema kuwa ameamua kutoa fedha hizo kutoka katika vitega uchumi vyake na amefanya hivyo kwa sababu suala hilo linamhusu yeye huku klabu yake ya Yanga ikiadhibiwa pasipo sababu.
“Nina magari na biashara zangu, nitalipa fedha hizo na nitarejea Jumamosi kucheza mechi yangu ya kwanza ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting, mpira ni kazi yangu na hili nimelifanya kutokana na mapenzi yangu ya dhati na Yanga,” alisema Ngassa.
Alisema kuwa hajisikii vizuri kukaa nje ya uwanja huku akiamini kuwa kipaji chake kinapotea. “Nimekaa nje, sikuwa na raha, sasa narejea kwa nguvu zote ili kuendeleza gurudumu la Yanga, mawazo yangu ya kucheza nje ya nchi kwa sasa nimeyafuta na hasa baada ya kupata ushauri kutoka kwa marafiki zangu, nawaomba radhi mashabiki na wanachama wa Yanga,” alisema Ngassa.
source: mwananchi newspaper