Saturday, 30 November 2013

MBWANA SAMATA NA THOMAS ULIMWENGU KUVAA MEDALI ZA DHAHABU LEO?


SAMATTA+SUPER+CUP+DRCWASHAMBULIAJI kutoka Tazania Mbwana Ally Samatta na Thomas Emanuel Ulimwengu leo watakuwa wanawania Medali za Dhahabu za michuano ya Afrika wakati klabu yao ya Tout Puissant Mazembe itakapokuwa inacheza na CS Sfaxien ya Tunisia hii itakua mara ya kwanza kwa Wachezaji wa kitanzania kuwania medali hizi.

TID AKAMATWA NA POLISI JANA USIKU.


Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed 'TID' yupo mahabusu katika Kituo cha Polisi Oysterbay tangu jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi msichana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake,  Mariam Nnauye.

AZAM YAMPA MKATABA WA MIAKA MIWILI KOCHA WA AKINA ETO’O



KLABU ya Azam leo imemtambulisha kocha wake mpya, Joseph Marius Omograia wa Cameroon iliyempa Mkataba wa miaka miwili kuanzia leo. Omog anatua Azam akitokea klabu ya A.C Leopards ya Kongo Brazavville ambayo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013) na kumaliza ukame wa mataji wa miaka 30. 
Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Mohammad kulia akimtambulisha kocha mpya, Omog katikati leo

MAPENZI NI NOUMA,,KIJANA AUKATA UUME WAKE KUEPUSHA USUMBUFU WA WANAWAKE HUKO TABORA.



Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimapenzi........ Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa nje
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu, aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.
Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za msingi.

Tuesday, 12 November 2013

P-FUNK 'MAJANI' APATA AJALI MBAYA AKIWA CHOONI....APASUKA KICHWANI NA KUSHONWA NYUZI 12


Paul Matthysse ‘P-Funk’ akionesha jeraha alilolipata kichwanibaada ya kuanguka chooni.
LEGEND wa kuzalisha mapigo ya muziki Bongo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, amepata ajali ya kushangaza chooni, nyumbani kwake, Mwenge Kijijini, Dar es Salaam.

HUU NDIO MJENGO MWINGINE WA DIAMOND AMBAO UPO KWENYE HATUA ZA MWISHO ILI KUKAMILIKA

Kijana anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz mambo si mabaya kwake baada ya kuonyesha mjengo wake mwingine wa hatari ambao bado upo katika ujenzi.  

 
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram,Diamond jana ame-share picha ya nyumba hiyo na chini akatia neno..Shuka nayo.

HII ALAMA YA VIDOLE 4 IMEMFANYA MCHEZAJI WA MISRI KUADHIBIWA.


Egypt 11
Unaambiwa club ya Al Ahly imemuadhibu mchezaji wake aitwae Ahmed Abdul Zaher kwa kitendo alichofanya cha kuonyesha alama za vidole kama unavyomuona hapo chini ikiwa ni ishara ambayo imekua ikitumiwa na wanaomuunga mkono rais Mohammed Morsi aliepinduliwa July 2013 na kwa sasa anakabiliwa na kesi ya kuchochea mauaji.

PICHA ZA DIAMOND AKIWA NIGERIA KUFANYA VIDEO YA NUMBER ONE REMIX NA MTU MZIMA DAVIDO


Anaitwa Mama Hilda,muigizaji mkongwe nchini Nigeria
                                           
Ni siku kadhaa sasa tangu 
niwasili nchini hapa,lengo likiwa ni moja tu,
          kuunganisha music wetu na wenzetu wa Nigeria,nitashoot video
 ya number one remix
                                    with my nicca Davido ,pamoja na kumalizia kazi niliyofanya 
na mwanamziki mwingine wa hapa 
                               Nigeria..kikubwa ni kuendeea kuwapa mashabiki zangu kile haswa                 mnachokistahili kutokana na sapoti kubwa
 mnayoendelea kunipa..

JANGA JINGINE NCHINI UFILIPINO,WATU ZAIDI YA 10,000 WANAHOFIWA KUFARIKI.

017217323_35400_2f32e.jpg
Wanajeshi na polisi wa Ufilipino wamepelekwa katika miji ilioathirika na kimbunga kikali kuwahi kuipiga nchi hiyo ili kudhibiti wizi wa mali unaohatarisha juhudi za kutoa misaada ya kibinaadamu kwa waathirika.

PICHA ZA MASTAAWANAPOJUTIA KUWA NA TATTOO MAMBO KAMA HAYA HUTOKEA


Producer Pharrell Williams alishawahi kukiri kuwa alipata maumivu makali sana wakati anafuta tatto alizochora wakati wa ujana wake na akajutia kitendo hicho. Alikuwa muoga wa magonjwa atakayopata baada ya tattoo kufutwa na mionzi mikali kwenye mwili wake inayoweza kusababisha saratani na magonjwa mengine.

Saturday, 9 November 2013

MANCHESTER UNITED V ARSENAL.OLD TRAFFORD KESHO,HIZI NDIZO TAKWIMU ZA TIMU HIZI


ARSENAL_TEAM-INDONESIAMAN_UNITED-DAVID_MOYES_BENCH
 Tayari Mechi 10 zimeshachezwa kwenye Ligi na Arsenal bado wanachanja mbuga wakiwa Tayari Mechi 10 zimeshachezwa kwenye Ligi na Arsenal bado wanachanja mbuga wakiwa hawajafungwa tangu wabamizwe 3-1 na Aston Villa kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu.

MOURINHO ALIA NA RATIBA LIGI KUU ENGLAND

MOURINHO-CHELSEA_TRAINING

 MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amedai Watu ambao wanatengeneza Ratiba ya Ligi Kuu England wanaicheka Timu yake.
Akiongelea kuhusu Mechi yao ya Ligi ya Jumamosi na West Bromwich Albion, Mourinho amelalamika kuwa kupewa Siku 3 toka Mechi yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Schalke waliyocheza Jumatano na kucheza tena Jumamosi wakati Klabu za Jiji la Manchester, Man United na Man City, na Arsenal zina Siku 4 toka Mechi zao za Ulaya sio sawa.

KLABU YA SIMBA YAWEKA WAZI USAJILI MPYA


julio_31d1c.jpg
SIMBA imepanga kuongeza kiungo mkabaji, beki wa kati na mshambuliaji kwenye dirisha dogo la usajili ingawa pia imedai itaangalia kwa jicho la tatu nafasi ya kipa inayoonekana kusuasua.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema nafasi hizo ndizo zimeonekana zina mianya.
Julio, ambaye kikosi chake kina wachezaji 26 alisema wanahitaji kujipanga upya na watawasilisha mapendekezo yao kwa uongozi.

Monday, 4 November 2013

MOYES AWATAKA MAREFA KUMLINDA JANUZAJ KAMA MESSI

KOCHA David Moyes amesema winga Adnan Januzai lazima alindwe na marefa baada ya Sascha Riether kuwa mchezaji wa kwanza kuadhibiwa chini ya sheria mpya baada ya marefa kutoona tukio uwanjani . 
Mshambuliaji huyo kinda alikuwa alichezewa rafu na beki huyo wa Fulham, United ikishinda 3-1 Uwanja wa Craven Cottage Jumamosi. 
Refa Lee Probert na wasaidizi wake hawakuona tukio hilo wakati linatokea, lakini marudio ya picha za video yanaonyesha vizuri. 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mlinzi: Marouane Fellaini akiwa na Adnan Januzaj, ambayealichezewa rafu na Sascha Riether Jumamosi

HII NDIYO NYUMBA YENYE THAMANI YA DOLA MILLION 48,INA UWANJA WA NDEGE HAPO HAPO NYUMBANI



article-2486741-1923386700000578-170_634x475
Nyumba hii ipo huko Las Vegas na ina acre 40 na indoor car parking kubwa sana kuingiza magari zaidi ya kumi kwa wakati mmoja. Upande wa mwingine ina zoo humohumo ndani,jet inayopark kwenye airport yako binafsi hapo mjengoni haina haja ya kwenda kwenye public airport. Ukitaka kumiliki hii nyumba inabidi zikutoke $ 48 millioni.

Saturday, 2 November 2013

MASHABIKI SIMBA WATAKA WACHEZAJI WAKONGWE WARUDISHWE

mashabiki_wa_simba_wakifurahia_ushindii_dc4d7.jpg
MASHABIKI WA SIMBA 
Mashabiki Simba wamepiga kelele na kutala benchi lao la ufundi libadilike na kuwarudisha wachezaji wakongwe.

PINDA, MAWAZIRI HATARINI KUNG'OLEWA


Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na mawaziri wake wawili; Khamisi Kagasheki (Maliasili na Utalii) na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk Mathayo David wameingia matatani kutokana na shinikizo linalowataka wang’oke katika nafasi zao.

DIAMOND AUTIBUA MSAFARA WA RAIS


STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Alhamisi iliyopita alijikuta akiutibua msafara wa Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein kufuatia kuondoka kwenye msiba wakati ilitangazwa kiongozi huyo ndiye aliyetakiwa kuanza kuondoka

Friday, 1 November 2013

LEWANDOSKI ATUMA SALAMU KWA ARSENAL! APIGA HETITRIKI, DORTMUND YAIBONDA STUTTGART 6-1!

Robert Lewandowski amepiga Bao 3 wakati Borussia Dortmund ilipotoka nyuma na kuibamizaStuttgart Bao 6-1 na kutua kileleni mwa Bundesliga.
Karim Haggui aliifungia Stuttgart Bao lao mapema lakini Sokratis Papastathopoulos akasawazisha kwa kichwa na Marco Reus kufunga Bao la pili kwa Dortmund.
Ndipo zikaja Bao 3 za Lewandowski na Pierre-Emerick Aubameyang kumalizia Bao la 6.

LIGI KUU UINGEREZA NI PATASHIKA JUMAMOSI HII EMIRATES, ARSENAL v LIVERPOOL!

>>WENGER ANAAMINI GIROUD NI KIBOKO KUPITA ‘SAS’, SUAREZ & STURRIDGE!
>>CHELSEA KUFUNGUA JUMAMOSI ST JAMES PARK NA NEWCASTLE!!
>>MABINGWA MAN UNITED NDANI YA CRAVEN COTTAGE NA FULHAM!!
>>MAN CITY: KIPA JOE HART BENCHI…. PANTILIMON NAMBA 1!!
RATIBA
Jumamosi Novemba 2
[Saa za Bongo]
1545 Newcastle v Chelsea

1800 Fulham v Man Utd

1800 Hull v Sunderland

1800 Man City v Norwich

KOBE HUYU ANAVUTIA SIGARA 10 KWA SIKU



Meet-A-Turtle-That-Smokes-10-Cigarettes-A-Day.jpg2
Maajabu hayaishi duniani na kila siku yanajitokeza maajabu mapya ambayo hukuwahi kutarajia kuyashuhudia maishani mwako . Nchini Japan kuna kobe ambaye amejiingiza kwenye tabia ya uvutaji wa sigara na mpaka sasa anavuta sigara kumi kwa siku.

YANGA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI, YAICHAPA JKT RUVU 4 - 0.YAPAA MPAKA NAFASI YA KWANZA.


Kikosi cha Young Africans kilichoanza leo dhidi ya JKT Ruvu

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Young Africans leo imekamata kiti cha uongozi baada ya kuendeleza wimbi la ushindi mfululizo kwa kuichapa timu ya Maafande wa jeshi la Kujenga Taifa nchini JKT Ruvu kutoka mkoani Pwani kwa mabao 4- 0 mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kikosi cha mholanzi Ernie Brandts kiliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha kinapata pointi 3 muhimu , jambo ambalo vijana wake walilitekeleza na kuwapa furaha washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Yanga waliokwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo.
 
Mshambuliaji Mrisho Ngassa aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 3 ya mchezo kwa shuti kali baada ya kuwatoka walinzi wa JKT Ruvu na kumtazama amekaa vipi mlinda mlango wa JKT Ruvu na kuukwamisha mpira wavuni.
 
Dakika ya 12 ya mchezo, Mrisho Ngassa tena aliwainua vitini mashabiki wa timu ya Young Africans baada ya kumalizia mpira ulipogwa na Saimon Msuva kabla ya kuwababatiza walinzi wa JKT Ruvu na kumkuta mfungaji ambaye aliukwamisha mpira wavuni kwa kichwa.
 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, JKT Ruvu 0 - 2 Young Africans .
 
Kipindi cha pili cha mchezo ulianza kwa kasi na Young Africans kupata bao la tatu la mchezo dakika ya 47 kupitia kwa Oscar Joshua ambaye alikutana na mpira uliokolewa walinzi wa JKT na kumkuta mfungaji ambaye alifunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na klabu ya Yanga miaka mitatu iliyopita.
 
Mabadiliko yaliyofanya na kocha mholanzi Ernie Brandts kuwaingiza Reliants Lusajo, Ibrahim Job na Jerson Tegete yaliongeza kasi na uwezo wa kumiliki mchezo kwani waliweza kucheza vizuri na kulilinda lango lao lisipatwe na madhara yoyote.
 
Dakika ya 89 Jerson Tegete aliipatia Yanga bao la nne la mwisho katika mchezo huo kufuatia migongeo ya Saimon Msuva na Ngassa kabla ya kumkuta Tegete akiwa peke yake na kuukwamisha mpira wavuni.
 
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, JKT Ruvu 0 - 4 Young Africans

Young Africans: 1.Dida, 2.Twite/Job, 3.Oscar, 4.Cannavaro 5.Yondani/Lusajio, 6.Chuji 7.Msuva 8.Domayo, 9.Kavumbagu/Tegete, 10.Ngassa, 11.Kiiza