Klabu
ya Manchester United imetajwa kuwa tayari kusikiliza ofa mbalimbali
ziotakazokuja kwa ajili ya winga Ashley Young baada ya mchezaji huyu
kushindwa kumridhisha kocha wa United David Moyes ambapo Ashley amekuwa
kwenye kiwango cha chini tangu msimu huu ulipoanza na amekuwa moja ya
watu wanaolalamikiwa sana na mashabiki wa United kwa kuonyesha kiwango
cha chini.
Zaidi
ya hapo kocha wa United David Moyes anaonekana kukerwa na tabia ya
winga huyu ya kujiangushaangusha akiwadanganya waamuzi ili wampe penalty
kama ilivyokuwa kwenye mchezo kati ya United na Crystal Palaca mapema
msimu huu.
Manchester
United inatarajiwa kufanya usajili mwezi January lakini mpango huo pia
utahusisha baadhi ya wachezaji ambao wanatarajiwa kuondoka United ambao
orodha yake pia inamjumuisha kiungo wa Japan Shinji Kagawa ambae
ameshindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza tangu David Moyes alipoanza
kazi kama kocha wa United.
No comments:
Post a Comment