KLABU ya Manchester United imempa Adnan Januzaj ofa ya mshara wa Pauni 60,000 kwa wiki ili abaki Old Trafford baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda Uwanja wa Light.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, zao
lingine la kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji, alicheza mechi yake ya
kwanza ya Ligi Kuu ya England na kufunga mabao mawili yalioyomfariji
kocha David Moyes kwa ushindi wa 2-1.
Na wakati mkataba wa mshambuliaji huyo
unamalizika miezi nane ijayo, klabu kadhaa zimeonyesha nia ya kumsajili,
hivyo kocha huyo United anataka kumbakiza nyoa wake huyo mpya.
![Tempting: Manchester United have offered Adnan Januzaj £60,000 per week to stay at the club](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/10/06/article-0-188B8F9E00000578-926_634x456.jpg)
Kifaa: Manchester United imempa Adnan Januzaj ofa ya mshahara wa Pauni 60,000 wiki abaki katika klabu hiyo
![On the town: Januzaj takes a stroll through Manchester on Sunday afternoon](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/10/07/article-2447175-18903F7A00000578-324_634x1293.jpg)
Mitaa ya mjini: Januzaj akitalii mitaa ya Jiji la Manchester Jumapili
![Adnan Januzaj](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/10/06/article-2447175-188BB29C00000578-986_634x544.jpg)
Kazi nzuri imefanyika: Januzaj akipongezwa na wenzake Robin van Persie na Michael Carrick baada ya kufunga
![Praise: Wayne Rooney is a fan of the precocious talent](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/10/07/article-2447175-188BB57200000578-311_634x443.jpg)
Wanamkubali: Wayne Rooney ni shabiki mkubwa wa nyoa huyo mwenye kipaji
![Adnan Januzaj](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2013/10/06/article-2447175-188BB04C00000578-702_634x406.jpg)
: Kocha wa United,
David Moyes amempa nafasi Januzaj kung'ara kama alivyofanya kwa Rooney
alipokuwa naye Everton
No comments:
Post a Comment