Vikosi vya usalama nchini Misri
vimeimarisha ulinzi katika sehemu kadhaa mjini Cairo baada ya vurugu
kuzuka kutokana na makabiliano kati ya wafuasi wa Mohammed Morsi na
vikosi vya usalama katika mji huo na ule wa Alexandria.
Milipuko na milio mikubwa ya risasi imesikika katika sehemu
za katikati mwa mji mkuu.
Pia usalama umeimarishwa karibu na medani ya Tahrir ambako waandamanaji waliokuwa wanapinga Morsi walikusanyika katika maandamano ya kumtaka ajiuzulu kabla ya majeshi kumtoa madarani miezi mitatu iliopita.
Vyombo vya habari vimeripoti kutokea ghasia zaidi katika mkoa wa Kaskazini wa Sharqiya, Mashariki mwa Giza, pamoja na Kaskazini mwa mji wa bandarini wa Alexandria.
Mamia ya watu wameuwa tangu jeshi kumuondoa mamlakani Morsi mwezi Julai.
Maelfu ya wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood pia wamezuiliwa katika miezi miwili iliopita.
Baadhi ya maafisa wakuu wa chama hicho akiwemo bwana Morsi na generali Mohammed Badie, wanazuiliwa kwa madai ya kuchochea ghasia na mauaji.
Vuguvugu hilo limelalamika na kusema kuwa maafisa wanazifanya juhudi zao dhidi yaokuonekana kama vita dhidi ya ugaidi
No comments:
Post a Comment