![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/02/16/120216082423_herve_renard_304x171_reuters_nocredit.jpg)
Kocha Herve aliiongoza Chipolopolo kushinda kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2012
Zambia imempa idhini kocha Herve
Renard kuyaacha majuku yake katika timu ya taifa ya nchi hiyo ili
kuchukua jukumu lake jipya la kuwa kocha wa timu ya ufaransa ya FC
Sochaux.
Kocha huyo alikuwa ameanza muhula wa pili wa
mkataba wake kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia mnamo mwezi Oktoba
mwaka 2011 na kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa kombe la mataifa ya
Afrika miezi minne baadaye.Beaumelle, amekuwa akifanya kazi kama kocha wa muda, na atashikilia wadhifa wa kocha mkuu wakati Chipolopolo watapocheza mechi ya kirafiki na Brazil mjini Beijing tarehe 15 Oktoba.
Shirikisho la soka nchini humo katika taarifa yake lilisema kuwa kocha "Herve Renard ameachishwa majuku yake ili kumruhusu kuiongoza timu ya Ufaransa.''
Renard, mwenye umri wa miaka 45, alichukua wadhifa huo wa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zambia mwaka 2008 na aliiongoza timu hiyo hadi kufika robo fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2010.
Baadeya alikuwa kocha wa timu ya Angola na USM Alger kwa muda kabla ya kurejea kuwa kocha wa Zambia na kutimiza ndoto yake ya kuiongoza Zambia kunyakua kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment