Sunday, 20 October 2013

LULU AONYESHA USHABIKI WA KWELI,NI BAADA YA MECHI YA SIMBA NA YANGA KUMALIZIKA KWA MAGOLI 3 - 3,


lulu3
Mechi ya leo kati ya Simba na Yanga ilianzia kwenye mitandao ya kijamii na baada ya mechi mambo yanaendelea kwenye mitandao tena. Muigizaji Lulu ameonyesha waziwazi upande wake anaoshabikia kwa kuandika maneno haya kwenye account yake ya instagram.


“Naomba tuelewane jamani…wala hatushangilii droo. Bali tunashangilia ushujaa wetu wa kurudisha zile 3. Tuelewane jamani, ukitaka kuona ule ni ushujaa angalieni mlivyokosa raha, kwani si droo!??, kwanini mnune. Bwahahaha…me bado natuma salamu zangu kwenu watani wangu. Kama nawapenda hvi..Oky bye.”
lulu
Kabla ya hapo pia ali-post logo ya Simba sports club na kuandika caption ya “Natuma salamu zangu kwa watani wangu wa jadi kwa kutangulia na gari la udongo wakati mbele ya safari kulikuwa na mvua. Oky By.
Hii pia ni post baada ya matokeo ya mechi kwenye facebook page ya shabiki mkubwa wa Simba Zitto Kabwe
zito

No comments:

Post a Comment