Baada
ya bosi wa washika mitutu wa jiji la London Arsene Wenger kumuonya
kiungo wake Jack Wilshere ambaye alikataa katakata juu ya mwenendo wake
wa hovyo wa kuvuta sigara mbele ya hadhira, hatimaye kiungo huyo
amekubali kosa na kuahidi kuwa haitatokea tena.
Wilshere
amesema kuwa alifanya kosa baada ya kupigwa picha akivuta sigara nje ya
ukumbi mmoja wa starehe huko London mida ya usiku.
Bosi
wa Wenger aliweka hilo wazi Ijumaa iliyopita ambapo alikaririwa akisema
hakubaliani hata kidogo na tabia hiyo na licha ya awali kiungo huyo wa
kimataifa wa England kukanusha, sasa amekubali kufanya kuhukumiwa kwa
kosa hilo.
Akiongea na mtandao wa klabu hiyo Wilshere amenukuliwa akisema
"I made a mistake,"
"Players make mistakes. I'm not a smoker.
"Nimeongea na bosi na kunitaka kueleza kilichotokea na nimemueleza na hatimaye kutatua hilo na kunirejesha kikosini na nina matumaini na kumjibu kwa kufunga goli dhidi ya West Brom.
"Haitatokea tena, mimi si mvuta sigara hivyo nadhani hiyo itakuwa ni mara ya mwisho."

No comments:
Post a Comment