Toka kipindi ameanza kuwa staa, Mcanada huyu mwenye umri wa miaka 19 matukio yake hayakua yenye utofauti sana na picha ambayo wengi walikua nayo kichwani kuhusu yeye akiwa ni staa mdogo anaejua kuvaa kisasa lakini bila kuvuka mipaka na kutoonekana kama mastaa wengine waliolewa sifa.. ila kwa sasa baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikimuonyesha na hata kuripoti stori zake za misukosuko ikiwemo kutukana waandishi wa habari na kutaka kuwapiga.
Kwenye tukio ambalo limefanya hii post iwepo hapa ni kuhusu yeye kuonekana kwenye moja kati ya club za usiku ambazo sehemu kubwa ya vinavyopatikana ndani ni pamoja na kina dada maalum kucheza wakiwa na nguo chache au wakati mwingine kutoaa kabisa. (Texas strip club)
Kilichofanya mpaka Bieber aandikwe na TMZ ni pale picha yake ilipopatikana akiwa Texas Strip Club kifua wazi na pia suruali ikiwa chini kabisa na kufanya boxer yake kuonekana kwa sehemu kubwa, aina ya mavazi ambayo hakuwahi kuonekana nayo kipindi hicho.
Mmoja wa hao warembo wanaocheza bila nguo aliandika kwenye page yake ya twitter kwamba ‘Bieber aliyagusa makalio yangu, nimewahi kuwachezea mastaa wengi lakini hakuna hata mmoja amewahi kunigusa makalio kama alivyofanya Bieber, alinishtua sana’
No comments:
Post a Comment