![Kikosi cha Young Africans kilichoanza leo dhidi ya JKT Ruvu](http://www.youngafricans.co.tz/images/stories/vpljkt.jpg)
Kikosi cha Young Africans kilichoanza leo dhidi ya JKT Ruvu
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Young Africans leo imekamata kiti cha
uongozi baada ya kuendeleza wimbi la ushindi mfululizo kwa kuichapa timu
ya Maafande wa jeshi la Kujenga Taifa nchini JKT Ruvu kutoka mkoani
Pwani kwa mabao 4- 0 mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Kikosi
cha mholanzi Ernie Brandts kiliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha
kinapata pointi 3 muhimu , jambo ambalo vijana wake walilitekeleza na
kuwapa furaha washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Yanga
waliokwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo.
Mshambuliaji
Mrisho Ngassa aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 3 ya
mchezo kwa shuti kali baada ya kuwatoka walinzi wa JKT Ruvu na kumtazama
amekaa vipi mlinda mlango wa JKT Ruvu na kuukwamisha mpira wavuni.
Dakika
ya 12 ya mchezo, Mrisho Ngassa tena aliwainua vitini mashabiki wa timu
ya Young Africans baada ya kumalizia mpira ulipogwa na Saimon Msuva
kabla ya kuwababatiza walinzi wa JKT Ruvu na kumkuta mfungaji ambaye
aliukwamisha mpira wavuni kwa kichwa.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, JKT Ruvu 0 - 2 Young Africans .
Kipindi
cha pili cha mchezo ulianza kwa kasi na Young Africans kupata bao la
tatu la mchezo dakika ya 47 kupitia kwa Oscar Joshua ambaye alikutana na
mpira uliokolewa walinzi wa JKT na kumkuta mfungaji ambaye alifunga bao
lake la kwanza tangu ajiunge na klabu ya Yanga miaka mitatu iliyopita.
Mabadiliko
yaliyofanya na kocha mholanzi Ernie Brandts kuwaingiza Reliants Lusajo,
Ibrahim Job na Jerson Tegete yaliongeza kasi na uwezo wa kumiliki
mchezo kwani waliweza kucheza vizuri na kulilinda lango lao lisipatwe na
madhara yoyote.
Dakika
ya 89 Jerson Tegete aliipatia Yanga bao la nne la mwisho katika mchezo
huo kufuatia migongeo ya Saimon Msuva na Ngassa kabla ya kumkuta Tegete
akiwa peke yake na kuukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, JKT Ruvu 0 - 4 Young Africans
Young Africans: 1.Dida, 2.Twite/Job, 3.Oscar, 4.Cannavaro 5.Yondani/Lusajio, 6.Chuji 7.Msuva 8.Domayo, 9.Kavumbagu/Tegete, 10.Ngassa, 11.Kiiza