![](http://a.files.bbci.co.uk/worldservice/live/assets/images/2014/08/26/140826095505_russian_soldiers_ukraine__512x288_ukraynasavunmabakanligi.jpg)
Friday, 29 August 2014
Tuesday, 26 August 2014
PHIRI ATAKA UGUMU WA MECHI SIMBA UENDE UNAONGEZEKA
PHIRI AKIWA MAZOEZINI NA AMRI KIEMBA |
BARUA YA DI MARIA YAWAACHA NA MAJONZI WACHEZAJI, MASHABIKI WA REAL MADRID
GIGGS AANGUA KILIO BENCHI ,,,,MAN UNITED IKIPIGWA 4-0 NA KITIMU CHA 'MCHANGANI' USKU HUU
DI MARIA ASAINI MAN UNITED, VAN GAAL AMKABIDHI JEZI YEYE MWENYEWE
KIBALI CHAMKWAMISHA BEKI MPYA KUANZA KAZI MAN UNITED
Wanajeshi wa Urusi walikuwa Ukraine kimakosa
![](http://a.files.bbci.co.uk/worldservice/live/assets/images/2014/08/26/140826095505_russian_soldiers_ukraine__512x288_ukraynasavunmabakanligi.jpg)
RONALDO NA BENZEMA WOTE WAFUNGA REAL IKIIANZA LA LIGA KWA USHINDI WA 2-0 NYUMBANI
Mwanzo mzuri; Cristiano Ronaldo jana amefunga katika ushindi wa kwanza wa Real msimu mpya wa La Liga |
Monday, 25 August 2014
SURE BOY AREJESHWA KIKOSINI
KIUNGO wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure
Boy’ amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akiitwa
kwa mara ya kwanza chini ya kocha Mholanzi,
Mart Nooij.
Nooij ametaja kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili
ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya
Morocco utakaochezwa Septemba 5, mwaka huu
nchini Morocco.
Wachezaji wengine wapya katika kikosi hicho
kutoka kile kilichotolewa na Msumbiji katika
mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika
ni kiungo Said Ndemla wa Simba SC na
washambuliaji Mwagane Yeya wa Mbeya City na
Juma Luizio wa ZESCO United ya Zambia.
Kikosi kamili ni makipa; Deogratias Munishi
(Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said
Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari
Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin
Yondani (Azam), Aggrey Morris (Azam), Joram
Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto
(Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba),
Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam),
Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na
Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis
Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana
Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa
(Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma
Liuzio ZESCO, Zambia).
Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini
Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika
hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na
kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam.
TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA..DIMARIA UYOO MAN U
Manchester United wamekamilisha majadiliano
na Real Madrid na watalipa pauni milioni 63.9
na kuvunja rekodi ya Uingereza kumnunua
winga Angel Di Maria (Sky Sports), mchezaji
huyo kutoka Argentina huenda akafikia kuuzwa
kwa pauni milioni 72, milioni 60 zikilipwa
mwanzo na milioni 12 baadaye (Daily Mirror),
Juventus wataanza mazungumzo na Arsenal
kuhusu Lukas Podolski. Juventus wanamtaka
kwa mkopo lakini Arsenal wanataka kumuuza
(Daily Telegraph), boss wa Real Madrid Carlo
Ancelotti amesema Sami Khedira, 27,
hatoondoka licha ya kufuatiliwa na Arsenal,
Bayern Munich na Manchester United
(Guardian), meneja wa Everton Roberto
Martinez amesema bado anaweza kumsajili
Samuel Eto'o, 33, au Danny Welbeck, 23, katika
wiki ya mwisho ya dirisha la usajili (Times),
boss wa Arsenal Arsene Wenger amemuulizia
beki mkabaji wa Brazil Luiz Gustavo, 27,
anayechezea Wolfsburg (Daily Mirror),
Southampton wamepanda dau kwa winga wa
Tottenham Andros Townsend, 23, (ESPN FC),
meneja wa Southampton Ronald Koeman yuko
tayari kuanza kumfuatilia tena winga wa
Norwich Nathan Redmond, 20, (Sun), Liverpool
watalazimika kuchukua hatua za haraka
kumsajili Radamel Falcao, 28, wakati Juventus
wakimtaka mshambuliaji huyo wa Monaco kwa
mkopo (Daily Star), Fernando Torres
hatoondoka Chelsea bila ya mkataba wa kitita
cha pauni milioni 8.5 kutolewa. Roma
wanamtaka mshambuliaji huyo (Sun),
Sunderland wamekuwa na mazungumzo na
winga wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou,
29, ambaye pia anatazamwa na Arsenal,
Liverpool na Everton (Daily Express), boss wa
Sunderland ana matumaini ya kupata jibu
iwapo mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini,
23, atajiunga nao au la (Sunderland Echo), West
Ham wamemuulizia beki wa Manchester City
Micah Richards, 26, ambaye anaonekana
huenda akaondoka City wiki hii (Sun), QPR
wamehusishwa na kipa wa Reading Alex
McCarthy, 24, (Daily Star), AC Milan
wanamtaka Samuel Eto'o na Fernando Torres
kuziba pengo la Mario Balotelli (Gazetta dello
Sport), Juventus wana nafasi kubwa ya
kumshawishi Radamel Falcao kujiunga nao kwa
mkopo wa mwaka mmoja (Gazetta dello Sport),
Lukas Podolski huenda akasaini mkataba wa
miaka mitatu na Wolfsburg na watalipa euro
milioni 12 kumsajili kutoka Arsenal (L'Equipe).
Zimesalia siku saba kabla ya dirisha la usajili
kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Cheers!!!!
TANZANIA KUANDAA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA BAADA YA LIBYA KUJITOA
TANZANIA itaomba kuandaa Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017, kufuatia
Libya kujitoa.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ameiambia KITOMIXNEWS leo
kwamba wana uwezo na wako tayari kuwa
wenyeji wa fainali hizo- hivyo wataomba.
“Tutaomba kuwa wenyeji wa AFCON ya 2017
kuziba pengo la Libya, tuko tayari na tuna
uwezo, tunatarajia sapoti kubwa ya Serikali na
wadau wengine wa Tanzania katika
hili,”amesema Malinzi.
Libya imeamua kujitoa kutokana na vurugu za
kisiasa zinazoendelea nchini humo- hivyo
kuhofia mazingira ya kiusalama.
Awali, Libya ilipewa uenyeji wa fainali za mwaka
2013, lakini ikajitoa kwa sababu kama hizo na
Afrika Kusini ikapewa nafasi hiyo- huku
makubaliano yakifikiwa wao wataandaa AFCON
ya mwaka 2017.
Jumamosi ikatangazwa tena, Libya imejitoa
baada ya viongozi wa nchi hiyo kukutana na
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa
Hayatou.
CAF ikasema jitihada za kumsaka mbadala wa
Libya zinaanza mara moja- maana yake
kujitokeza kwa Tanzania ni ahueni kwao.
Kwa sasa, Tanzania inaweza kabisa kuwa
mwenyeji wa fainali hizo kwa kuwa ina viwanja
visivyopugua vitatu vyenye sifa, ingawa vingine
vitahitaji marekebisho madogo.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hakuna shaka
una sifa zote, wakati CCM Kirumba mjini
Mwanza na Sheikh Amri Abeid Arusha vitahitaji
marakebisho kidogo.
Iwapo Tanzania itafanikiwa kupata uenyeji wa
fainali za mwaka 2017, itakuwa imefuzu moja
kwa moja kucheza michuano hiyo bila kupitia
kwenye hatua ya mchujo.
Na hiyo itakuwa mara ya pili kihistoria kushiriki
AFCON baada ya 1980 mjini Lagos, Nigeria
wakati huo bado michuano hiyo ikiitwa Kombe la
Mataifa ya huru ya Afrika.
Tanzania ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji
Nigeria, Ivory Coast na Misri na ikashika mkia.
Ilifungwa 3-0 na Ngeria, 2-1 na Misri na kutoka
sare ya 1-1 na Ivory Coast.
Yapo matumaini makubwa Tanzania ikafanikiwa
kupewa yenyeji wa michuano hiyo mwaka 2017,
kutokana na uhusiano mzuri baina ya Hayatou
na rais wa sasa wa TFF, Malinzi. Kwa ujumla,
FIFA na CAF zina imani kubwa na utawala wa
Malinzi.
Wednesday, 20 August 2014
PHIRI AWAKUMBUKA KASEJA, YONDANI AKIWA ZANZIBAR
ROJO ATUA MAN UNITED KUKAMILISHA USAJILI
JULIO CESAR ATUA BENFICA MIAKA MIWILI BAADA YA KUPOTEZA NAMBA QPR
Saturday, 16 August 2014
ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, SPURS NAYO YAUA MTU
BAO la dakika ya 90 na ushei la Aaron Ramsey
limeipa mwanzo mzuri Arsenal katika Ligi Kuu ya
England, baada ya kuichapa 2-1 Crystal Palace
kwenye Uwanja wa Emirates, London.
Ilibaki kidogo tu Gunners kuanza kwa sare baada
ya Crystal kutangulia kupata bao kupitia kwa
Brede Hangeland dakika ya 35 kabla ya Laurent
Koscielny kuisawazishia Arsenal dakika ya 45 na
ushei.
Refa Jon Moss alimtoa nje kwa kadi ya pili ya
njano na kuwa nyekundu Jason Puncheon wa
Crystal Palace dakika ya 88 baada ya
kumchezea rafu Monreal.
Kikois cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Debuchy,
Chambers, Koscielny, Gibbs/Monreal dk53,
Wilshere/Oxlade-Chamberlain dk69, Arteta,
Sanchez, Ramsey, Cazorla, Sanogo/Giroud dk62.
Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann/Delaney
dk75, Hangeland, Ward, Puncheon, Jedinak,
Ledley, Bolasie/O'Keefe dk90, Chamakh na
Campbell/Gayle dk85.
Katika mechi nyingine za ufunguzi leo Ligi Kuu
England, Stoke City imelala nyumbani 1-0 mbele
ya Aston Villa, bao pekee la Andreas Weimann
dakika ya 50 Uwanja wa Britannia, Leicester City
imetoka sare ya 2- 2 na Everton, Queens Park
Rangers imefungwa 1-0 nyumbani na Hull City,
bao pekee la James Chester dakika ya 52
Uwanja wa Loftus Road,
West Bromwich Albion imetoka 2-2 na
Sunderland Uwanja wa The Hawthorns, West
Ham United imefungwa 1-0 nyumbani na
Tottenham Hotspur bao pekee la Eric Dier dakika
ya 90 na ushei Uwanja wa Boleyn Ground, wakati
Manchester United imefungwa 2-1 nyumbani na
Swansea City.
VAN GAAL ASEMA KIPIGO CHA KIJANA KITAPOTEZA KUJIAMINI MAN UNITED, AKIRI PIA IPO HAJA YA KUSAJILI, HASWA MABEKI
KOCHA Louis van Gaal amesema kwamba
kujiamini kwa Manchester United itaondoka
baada ya kipigo cha jana cha mabao 2-1 katika
mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England
nyumbani mbele ya Swansea.
Bao la Gylfi Sigurdsson dakika ya 72 lilimvuruga
kocha mpya wa United, Van Gaal kuftia ushindi
mfululizo katika mechi sita za kujiandaa na
msimu, Mashetani hao Wekundu wakifungwa
kwa mara ya kwanza nyumbani katika mchezo
wa ufunguzi ndani ya miaka 42.
"Unaposhinda kila kitu katika wakati wa
maandalizi na kuja kufungwa mechi ya kwanza,
hiyo haiwezi kuwa mbaya," amesema.
"Tumejijengea hali ya kujiamini kwa kiasi
kikubwa na kisha itaondoka kwa sababu ya
matokeo haya,".’
Mwanzo mbaya: Louis van Gaal akiondoka
uwanjani jana baada ya Manchester United
kuchapwa na Swansea
Mholanzi huyo alilazimika kuwachezesha kwa
mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya England
Jesse Lingard na Tyler Blackett, akiwa amesaini
wachezaji wawili tu wapya— Ander Herrera na
Luke Shaw msimu huu.
Alipoulizwa kama kipigo hicho kitamlazimu
kuingie sokoni kusajili kuboresha kikosi, Van Gaal
alisema: "Nilifikiri hivyo mkabla ya mechi hii,
hivyo hakuna tofauti. Wakati tunacheza
Marekani niliona kama hivyo. Kweli tunahitaji
mabeki. Lakini huwezi kusema hivyo, kwa
sababu tumepoteza mechi moja na tumeshinda
nyingine zote, hiyo ni beki. Ni timu ambavyo
tumecheza,".
Katika staili yake maarufu, Van Gaal, Mholanzi
hiyo hakumnyooshea kidole yeyote baada ya
mechi. Kocha huyo mpya wa United, aliwalaumu
wachezaji wake kwa kucheza ovyo. Pia alisema
walikosa hali ya kujiamini na hawakucheza
kitimu.
"Ni siku mbaya sana kwetu. Imewaangusha sana
wachezaji, mashabiki, mimi, na
viongozi,"alisema.
LIGI KUU ENGLAND YAANZA LEO, MAN UNITED YA VAN GAAL, CHELSEA YA MOURINHO YENYE DIEGO COSTA, LIVERPOOL BILA SUAREZ, ARSENAL MPYA NA MABINGWA MAN CITY…PATAMU HAPOO!
LIGI KUU ya England inaanza leo na Louis van
Gaal anaanzisha rasmi zama mpya Manchester
United atakapoiongoza dhidi ya Swansea City
Uwanja wa Old Traffford.
Mwalimu huyo wa Kiholanzi mwenye umri wa
miaka 63 amefanya vizuri katika wiki zake nne
za kwanza United, akiiwezesha timu kushinda
mechi tano na sare moja katika mech za
kujiandaa na msimu na sasa watu wanataka
kuangalia mafanikio yake katika ligi.
Swansea ni moja kati ya timu nane ambazo
msimu uliopita zilishinda mechi Old Trafford
Mashetani Wekundu wakiwa chini ya kocha
David Moyes aliyetupiwa virago kwa matokeo
mabaya mwishoni mwa msimu.
Ikumbukwe, United pia ilikutana na Swansea
katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu huo
2013-2014 wakiwa mabingwa watetezi na
kushinda mabao 4-1 Uwanja wa Liberty, siku za
mwanzoni za Moyes kazini.
Matokeo hayo hayakuwa na maana, kwani
mwishoni mwa msimu United ilimaliza katika
nafasi ya saba.
Wayne Rooney ataiongoza United kwa mara ya
kwanza tangu achaguliwe kuwa Nahodha
Jumanne timu hiyo ikishinda mabao 2-1 katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Valencia.
United itamkosa beki wake kinda wa kushoto
mwenye umri wa miaka 19 iliyemnunua kwa
Pauni Milioni 27, Luke Shaw, ambaye
anasumbuliwa na maumivu ya nyama.
Baada ya kuimarisha kikosi kwa kusajili nyota
kadhaa wapya, kocha Arsene Wenger ataiongoza
Arsenal katika mchezo wa ugenini dhidi ya
Crystal Palace.
Ikiwa imetoka kumaliza ukame wa miaka tisa wa
mataji kwa kushinda Kombe la FA msimu
uliopita, Arsenal ilifungua msimu vizuri kwa
kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifumua
Manchester City 3-0 wiki iliyopita.
Mchezaji mpya, Alexis Sanchez, aliyesajiliwa kwa
Pauni Milioni 30 kutoka Barcelona, anatarajiwa
kuwamo kwenye kikosi cha leo katika mchezo
wa kwanza wa ushindani sambamba na
Nahodha mpya, Mikel Arteta.
Palace inaingia katika mchezo wa leo ikiwa
katika mgogoro, kufuatia taarifa za kuondoka
kwa kocha Tony Pulis juzi baada ya kutofautiana
na wamiliki juu ya sera ya usajili.
Mabingwa wa Championship, Leicester City
watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu
England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha
Everton leo, wakati timu nyingine iliyopanda
msimu huu, Queens Park Rangers itaikaribisha
Hull City Uwanja wa Loftus Road.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City
wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle
United kesho.
Liverpool, iliyozidiwa kete na Man City katika
mbio za ubingwa msimu uliopita, wataanza
kampeni zao dhidi ya Southampton, ambao
wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na
Dejan Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield.
Lallana ataukosa mchezo huo kutokana na
maumivu ya goti, lakini Lambert na Lovren wote
wapo katika nafasi nzuri ya kuichezea Liverpool,
ambayo imetoka kumuuza kinara wake wa
mabao Luis Suarez kwa Barcelona.
Chelsea ya Mreno Jose Mourinho, ikiongozwa na
wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc
Fabregas itaifuata Burnley iliyoapanda msomu
huu Jumatatu.
Mechi nyingine; Stoke City na Aston Villa, West
Bromwich Albion na Sunderland na West Ham
United dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati kesho
Liverpool v Southampton, Newcastle United v
Manchester City na keshokutwa Burnley
Wednesday, 13 August 2014
Monday, 11 August 2014
BBC yazindua ofisi mpya Dar es Salaam
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/08/11/140811162415_bbc_studio_512x288_bbc_nocredit.jpg)
KOCHA BORA PATRICK PHIRI AJA DAR IJUMAA KUMWAGA WINO SIMBA SC KUREJESHA ENZI ZA MAFANIKIO MSIMBAZI
Sunday, 10 August 2014
Ndege nyingine yaanguka na kuua abiria wote
![q](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/q.jpg?resize=515%2C289)
Ndege ya kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makazi ya watu baada kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Magharibi mwa mji wa Tehran nchini Iran.
KAULI YA RAIS EVAVS AVEVA WA SIMBA KUHUSIANA NA KUTIMULIWA KWA LOGA HII HAPA
MAAJABU YA DUNIA,,JIONEE HUYU SAMAKI AMBAYE YUPO KAMA MTU..
![https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjYaVlyGuaBVGdvToxoN3D4838pbTJ9N0rRhQOc28AO9nuUXY-suNwe9nGk-Kfwsqmmqok8fq3guWaJE_Bi39Zj5aRSo08EM6qrrz5qJyhKOXiskCrKMOHxpN5BqAOagGC2PdS5gUw_8cAH/s1600/nguva.jpg](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjYaVlyGuaBVGdvToxoN3D4838pbTJ9N0rRhQOc28AO9nuUXY-suNwe9nGk-Kfwsqmmqok8fq3guWaJE_Bi39Zj5aRSo08EM6qrrz5qJyhKOXiskCrKMOHxpN5BqAOagGC2PdS5gUw_8cAH/s1600/nguva.jpg)
Hili ndilo bata refu la Serengeti Fiesta Mwanza lilivyokuwa.jionee picha hapa
Haya ndiyo mavazi wanayovaa wahudumu wa ndege kujikinga na Ebola
![3](http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/08/310.jpg?resize=467%2C268)
Saturday, 9 August 2014
EXCLUSIVE# DIAMOND PLATNUMZ LIVE AKIMLA DEN* WEMA NDANI YA ROCK CITY MWANZA...CHEKI HAPA
SIMBA SC YAPIGWA 3-0 NA KIONGERA WAO SIMBA DAY
DANNY MRWANDA ANA GARI AMBALO MCHEZAJI YEYOTE BONGO HANA, WANATUMIA VIGOGO NCHI HII
TETESI ZA SOKA ULAYA
Manchester United wametoa dau la pauni milioni 55 kumtaka kiungo wa Real Madrid Angel Di Maria, 26 (Daily Express), United pia watatazama kumchukua kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, kutoka Barcelona iwapo watashindwa kumpata Arturo Vidal, 27 (Daily Express), Borussia Dortmund wamesema watafanya kila wawezalo kubaki na kiungo wao Marco Reus, 25, licha ya mchezaji huyo kuwindwa na
Friday, 8 August 2014
VIFAA VYA SENEGAL, BOTSWANA VYATUA SIMBA SC
Simba imebakisha nafasi moja kukamilisha usajili wa wachezaji wa Kimataifa ambapo hadi sasa imeishasajili wachezaji Amis Tambwe, Joseph Owino, Kwizera Pierre na Modo Kiongore.
![]() |
Viongozi wa Simba SC wamepania kutengeneza kikosi kikali kuelekea msimu ujao |
GIGSS AIFUNGIA MAN UNITED YA WAKONGWE IKICHAPWA 5-1 NA KITIMU CHA DARAJA LA KWANZA
Ukweli kuusu Anti Ezekiel kutoka na dansa wa Diamond Platnumz.
‘Bunge la Katiba lisitishwe’
![](http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2412254/highRes/804935/-/maxw/600/-/13t1gqmz/-/bisimba.jpg)
UN yalaani mateso ya Wakristo Iraq
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/08/08/140808002539_iraq_640x360_reuters_nocredit.jpg)
Thursday, 7 August 2014
DIAMOND PLATINUM KUTUMBUIZA SIMBA DAY
Wednesday, 6 August 2014
Manchester United finally convince Vidal to join them at Old Trafford
Manchester United have finally reached a verbal agreement to sign Arturo Vidal according to El Mecurcio. There has been plenty of activity around the potential move with reports now suggesting a £48m and £200k a week deal is on the table in the Express and elsewhere.
MAN UNITED NA BAYERN MUNICH ZA MAGWIJI KUKUMBUSHIA FAINALI LA LIGI YA MABINGWA 1999
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIUYKjF0c_gaE_MQkKHzmZLKlpO3pJy8gw1VWBHRnABLAi2gjIZlxdjTbDjOnZ2u0EztIbc1CrQXhmTqSQRkYBq2yblmeYsqTvKw7qpIakIxZwqmzhyphenhyphenhcIji-isTVjes7cFODR-CdmnwKU/s1600/1407372658924_wps_7_Paul_Scholes_of_Mancheste.jpg)
Francois Nguema:Rais katili aliyeabudu uchawi-2
Linex nae kaweka nia ya kugombea ubunge,kwa kupitia chama hiki.
KARIM BENZEMA SASA 'KUZEEKEA' REAL MADRID
HOWARD WEB ATUNGIKA KIPYENGA, SASA BOSI WA MAREFA
Msichana aliyepigwa na mtoto wa Obama atoa kauli ya kushangaza
![Msichana aliyepigwa na mtoto wa Obama atoa kauli ya kushangaza](http://www.timesfm.co.tz/content/uploads/2014/8/5/cache/Malia%20Obama_full.jpg)
Warioba: Bunge litapoteza fedha za wananchi endapo hakuna maridhiano
![](http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2410174/highRes/803489/-/maxw/600/-/kwxqbk/-/bunge.jpg)
Tuesday, 5 August 2014
UKWELI KUHUSU KUACHANA NUH MZIWANDA NA SHILOLE HUU HAPA.
Ali Kiba: Lulu anafaa kuwa mke, aeleza kilichotokea siku ya kifo cha Kanumba
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya miaka 18!
Diamond Vs Ali Kiba : Nay wa Mitego atamani kutembeza kipigo kikali kukomesha
![Diamond Vs Ali Kiba : Nay wa Mitego atamani kutembeza kipigo kikali kukomesha (Audio)](http://www.timesfm.co.tz/content/uploads/2014/8/5/cache/Nay%20wa%20Mitego%20abt%20Ali%20Kiba%20Diamond_full.jpg)
Ushindani kati ya Diamond na Ali Kiba ambao siku zote mimi nauita ‘ushindani usio rasmi’ huku wengine wakiutafsiri kama ‘beef’ umetengeneza mitazamo tofauti kati ya wadau wa muziki Tanzania.
Ukweli kuhusu wimbo wa Linex: Zitto Kabwe ashiriki kukamilisha lyrics 70%, Adam Juma alipwa pesa ambayo hajawahi kulipwa na msanii yoyote, speech yake yaskika wishoni
BREAKING NEWS; YANGA SC YAENGULIWA KOMBE LA KAGAME, AZAM WACHUKUA NAFASI KIGALI
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiengua Yanga SC katika michuano ya Kombe la Kagame na nafasi hiyo kupewa Azam FC, zote za Tanzania.
Yanga SC imeenguliwa kwa sababu moja tu kubwa, kushindwa kuthibitisha kupeleka kikosi cha kwanza pamoja na kocha Mkuu, Marcio Maximo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.
Monday, 4 August 2014
Picha mpya ya mtoto wa Kanye West na Kim Kardasian yavutia watu mtandaoni.
VAN GAAL AREJESHA FURAHA MAN UNITED, YAWAFUMUA LIVERPOOL 3-1 NA KUBEBA MWALI WA KIMATAIFA MAREKANI
Saturday, 2 August 2014
NOOIJ APANGUA KIKOSI STARS, NGASSA NA OSCAR JOSHUA WAPIGWA MKEKA, MOURAD NA MCHA WANAANZA LEO DHIDI YA MAMBAS
![]() |
Tuko tayari; Kocha Mart Nooij akiwaongoza vijana wake kuingia Uwanja wa Zimopeto jana tayari kwa mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa leo |