Wednesday, 6 August 2014

KARIM BENZEMA SASA 'KUZEEKEA' REAL MADRID

Anabaki Bernabeu: Karim Benzema akiwa ameshika jezi yake namba tisa baada ya kuongeza mkataba Real Madrid 
 MSHAMBULIAJI wa kimataifa nwa Ufaransa, Karim Benzema ameongeza mkataba wa kuendelea kuichezea Real Madrid hadi mwaka 2019 baada ya kukataa kuhamia timu za Ligi Kuu ya England.
Kulikuwa kuna tetesi kwamba mpachika mabao huyo wa Ufaransa anaweza kuondoka klabu hiyo ya Hispania, lakini sasa wazi ataishi Bernabeu hadim mwaka 2019.
Arsenal, Liverpool na Tottenham Hotspur ni miongoni mwa timu za Ligi Kuu England zilizokuwa zinamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Staying put: Real Madrid forward Karim Benzema has committed himself to the club until 2019
Hapa ameshika jezi nyingine imeandikwa atakuwa Real Madrid hadi mwaka 2019

No comments:

Post a Comment