
MAGWIJI
wa Manchester United, Paul Scholes, Bryan Robson ana Edwin van der Sar
ni baadhi ya wachezaji wa zamani wa Mashetani hao Wekundu watakaocheza
mechi ya hisani dhidi ya nyota wenzao wa kitambo wa Bayern Munich
Jumamosi.
Mechi
hiyo itakayofanyika Uwanja wa Allianz Arena, itashuhudiwa mabingwa wa
sasa wa Bundesliga wakimenyana na wakali wanzao wa enzi hizo wa United.
Timu
hizo mbili zilikutana katika mechi kadhaa enzi zao, lakini zaidi
mpambano ambao bado upo kwenye kumbukumbu za wengi ni wa fainali ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya mwaka 1999, ambayo United ilishinda katika msimu
waliotwaa mataji matatu.

Kumbukumbu: Manchester United iliifunga Bayern Munich 2-1 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 1999
Paul
Breitner - aliyeiongoza Ujerumani Magharibi kutwaa Kombe la Dunia mwaka
1974 atakuwa Nahodha wa Bayern Munich ambayo itakuwa pia na wakali kama
Marc van Bommel na kiungo wa zamani wa United, Owen Hargreaves.
Kikosi
cha United pia kitahusisha wakali wa zamani kama Dwight Yorke, Andy
Cole, Ronny Johnsen na Quinton Fortune. Mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge amesema: "Nina uhakika litakuwa tukio moja maalum sana,".
Fedha zitakazopatikana katakana na mauzo ya tiketi zitakwenda katika mfuko wa kituo cha watoto cha Allianz.

Muuwaji: Andy Cole (kushoto), aliyeichezea Manchester United katika fainali ya mwaka 1999 atakuwepo pia
No comments:
Post a Comment