LIGI KUU ya England inaanza leo na Louis van
Gaal anaanzisha rasmi zama mpya Manchester
United atakapoiongoza dhidi ya Swansea City
Uwanja wa Old Traffford.
Mwalimu huyo wa Kiholanzi mwenye umri wa
miaka 63 amefanya vizuri katika wiki zake nne
za kwanza United, akiiwezesha timu kushinda
mechi tano na sare moja katika mech za
kujiandaa na msimu na sasa watu wanataka
kuangalia mafanikio yake katika ligi.
Swansea ni moja kati ya timu nane ambazo
msimu uliopita zilishinda mechi Old Trafford
Mashetani Wekundu wakiwa chini ya kocha
David Moyes aliyetupiwa virago kwa matokeo
mabaya mwishoni mwa msimu.
Ikumbukwe, United pia ilikutana na Swansea
katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu huo
2013-2014 wakiwa mabingwa watetezi na
kushinda mabao 4-1 Uwanja wa Liberty, siku za
mwanzoni za Moyes kazini.
Matokeo hayo hayakuwa na maana, kwani
mwishoni mwa msimu United ilimaliza katika
nafasi ya saba.
Wayne Rooney ataiongoza United kwa mara ya
kwanza tangu achaguliwe kuwa Nahodha
Jumanne timu hiyo ikishinda mabao 2-1 katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Valencia.
United itamkosa beki wake kinda wa kushoto
mwenye umri wa miaka 19 iliyemnunua kwa
Pauni Milioni 27, Luke Shaw, ambaye
anasumbuliwa na maumivu ya nyama.
Baada ya kuimarisha kikosi kwa kusajili nyota
kadhaa wapya, kocha Arsene Wenger ataiongoza
Arsenal katika mchezo wa ugenini dhidi ya
Crystal Palace.
Ikiwa imetoka kumaliza ukame wa miaka tisa wa
mataji kwa kushinda Kombe la FA msimu
uliopita, Arsenal ilifungua msimu vizuri kwa
kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifumua
Manchester City 3-0 wiki iliyopita.
Mchezaji mpya, Alexis Sanchez, aliyesajiliwa kwa
Pauni Milioni 30 kutoka Barcelona, anatarajiwa
kuwamo kwenye kikosi cha leo katika mchezo
wa kwanza wa ushindani sambamba na
Nahodha mpya, Mikel Arteta.
Palace inaingia katika mchezo wa leo ikiwa
katika mgogoro, kufuatia taarifa za kuondoka
kwa kocha Tony Pulis juzi baada ya kutofautiana
na wamiliki juu ya sera ya usajili.
Mabingwa wa Championship, Leicester City
watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu
England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha
Everton leo, wakati timu nyingine iliyopanda
msimu huu, Queens Park Rangers itaikaribisha
Hull City Uwanja wa Loftus Road.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City
wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle
United kesho.
Liverpool, iliyozidiwa kete na Man City katika
mbio za ubingwa msimu uliopita, wataanza
kampeni zao dhidi ya Southampton, ambao
wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na
Dejan Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield.
Lallana ataukosa mchezo huo kutokana na
maumivu ya goti, lakini Lambert na Lovren wote
wapo katika nafasi nzuri ya kuichezea Liverpool,
ambayo imetoka kumuuza kinara wake wa
mabao Luis Suarez kwa Barcelona.
Chelsea ya Mreno Jose Mourinho, ikiongozwa na
wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc
Fabregas itaifuata Burnley iliyoapanda msomu
huu Jumatatu.
Mechi nyingine; Stoke City na Aston Villa, West
Bromwich Albion na Sunderland na West Ham
United dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati kesho
Liverpool v Southampton, Newcastle United v
Manchester City na keshokutwa Burnley
Saturday, 16 August 2014
LIGI KUU ENGLAND YAANZA LEO, MAN UNITED YA VAN GAAL, CHELSEA YA MOURINHO YENYE DIEGO COSTA, LIVERPOOL BILA SUAREZ, ARSENAL MPYA NA MABINGWA MAN CITY…PATAMU HAPOO!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment