Francois Macias Nguema, alikuwa rais wa kwanza wa Guinea ya Ikweta kuanzia Oktoba 12, hadi Agosti 3, 1979. Nguema anakumbukwa kwa mengi katika utawala wake, lakini kubwa ni tabia yake ya kuamini ushirikina.
Kutokana na kuamini ushirikina kupita kiasi, wananchi wake walimuogopa kupinduki, kwani walishindwa hata kumsema pembeni wakidia kwamba anaweza kuwasikia.
Mbali na kuabudu imani za kishirikina, pia rais huyo anakumbukwa kutokana na ukatili kupindukia alioonyeshwa kwa watu wote walioonekana kutokukubalina na uongozi wake.
Jumuiya mbalimbali za kimataifa na zile za kutetea haki za binadamu zilimnyoshea kidole cha shahada kutokana na kuwaua wapinzani wake jinsi alivyotaka.
Kiongozi huyu hakuwa na uhuru hata kidogo dhidi ya wapinzani wake, aliwakamata na kuwaua, baadhi yao akiwatesa kupindukia na kisha kuamuru kuuawa.
Kibaya zaidi, ukatili wake ulivuka mipaka kwani hata wale marafiki zake wa karibu hakusita kuamuru wauawe pale alipobaini wanakwenda kinyume na maagizo yake.
Kwa kutumia uchawi aliodai kurithi kutoka kwa baba yake, alihifadhi mafuvu mengi ya vichwa vya binadamu alivyovitumia kama alama ya kuwatisha wapinzani wake.
Tofauti na nchi zingine ambako makazi ya rais huwa na walinzi mahiri, yeye kwake ilikuwa kinyume kidogo kwani aliwajaza wakuu wa kimila wa kabila lake na kushirikiana nao kufanya vitendo vya kishirikina.
Aliitumia pia Ikulu kama nyumba ya kufanyia vitendo vya uganga wa kutoa dawa na kufanya matambiko kwa watu waliokuwa na shida na kuomba msaada wake.
Mizimu yake ilimwaminisha kutunza pesa chini ya ardhi na mali zingine kama dhahabu na almasi. Sera zake za kibabe ziliwanyima raia wake maisha mazuri, kwani wengi walikuwa masikini kupindukia.
Guinea ya Ikweta ilipata uhuru wake, Oktoba 1968, lakini jambo la kushangaza siku 154 baadaye aligundua kuwa bendera ya wakoloni ilikuwa bado ikipepea katika maeneo kadhaa ya Guinea ya Ikweta, akaudhika.
Kutokana na hilo, aliagiza makundi ya mashabiki wake, vijana kuwashambulia wageni. Matokeo yake, raia 7,000 wa Hispania waliondoka nchini humo, wengi wakiwa watumishi wa umma.
Nafasi zao zikajazwa na watu wa kabila lake, Esangui. Wengi wao walikuwa ndugu zake, wapwa zake akiwamo Kanali Teadore Obiang Nguema Mbosogo, Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Taifa, kundi la kijeshi chini ya Fernando Po.
Kituko kikubwa alichowahi kufanya ni kulifuta neno usomi. Hakutaka neno hili kutumika, pengine kwa sababu yeye mwenyewe hakuwa msomi hivyo ni wazi kuwa dhamira yake ilikuwa ni kujenga taifa mbumbumbu kama alivyo.
Hatua ya kuzuia neno msomi kutumika ilikwenda sambamba na kufunga maktaba zote nchini mwake. Magazeti na viwanda vya uchapaji vikafungwa na elimu ikafa kabisa mwaka 1974.
Aliamuru dola kuweka picha zake kwenye makanisa yote akieleza kuwa yeye ni baba wa maajabu yote. Makasisi wakaamriwa kutangaza uongozi wake kuwa ndiyo Imani na kauli mbiu yake kubwa ilikuwa; “Hakuna Mungu mwingine zaidi ya Macias.”
Kati ya mwaka 1974-75, Nguema alizuia mikutano yote ya kidini, maziko na ibada nyinginezo. Majina ya wakristo yalifutwa. Aligeuza makanisa kuwa maghala. Alihifadhi silaha kwenye kanisa kuu mjini Malabo.
Kifo chake:
Septemba 1979 alipinduliwa na mpwa wake, Kanali Obiang Nguema baada ya kuhofia kuuwawa na rais huyo. baada ya kumpindua alimtia gerezani na
Nguema alikufa mwaka 1979. Alihukumiwa kifo na kupigwa risasi katika Gereza la Blabich mjini Malabo.
Kwa hofu ya uchawi wake, raia walikodi majeshi kutoka Morocco ambao walimpiga riasi.
No comments:
Post a Comment