KIUNGO wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure
Boy’ amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akiitwa
kwa mara ya kwanza chini ya kocha Mholanzi,
Mart Nooij.
Nooij ametaja kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili
ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya
Morocco utakaochezwa Septemba 5, mwaka huu
nchini Morocco.
Wachezaji wengine wapya katika kikosi hicho
kutoka kile kilichotolewa na Msumbiji katika
mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika
ni kiungo Said Ndemla wa Simba SC na
washambuliaji Mwagane Yeya wa Mbeya City na
Juma Luizio wa ZESCO United ya Zambia.
Kikosi kamili ni makipa; Deogratias Munishi
(Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said
Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari
Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin
Yondani (Azam), Aggrey Morris (Azam), Joram
Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto
(Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba),
Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam),
Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na
Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis
Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana
Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa
(Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma
Liuzio ZESCO, Zambia).
Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini
Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika
hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na
kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam.
Monday, 25 August 2014
SURE BOY AREJESHWA KIKOSINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment