Saturday, 2 August 2014

SAMATTA NA ULIMWENGU WATUA MAPUTO TAYARI KUUA MAMBA KESHO

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau kushoto akimlaki mshambuliaji Mbwana Samatta kulia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo, baada ya kuwasili asubuhi ya leo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji Msumbiji. 
Kidau akimlaki Thomas Ulimwengu kulia. Wachezaji hao wa TP Mazembe ya DRC wataichezea Taifa Stars kesho katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco.
Samatta, Ulimwenggu na Kidau wakizungumza. Stars ilitoa sare ya 2-2 na Mambas katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam, hivyo itahitaji ushindi wa ugenini ili kusonga mbele
Samatta na Ulimwengu wakiwa na Mtanzania anayeishi hapa, Ashraf

No comments:

Post a Comment