A.Y
akiwa na wasanii wengi wakubwa kutoka Africa wamesafiri pamoja na
mchezaji wa Manchester city “Yaya Toure” kwenda Washington D.C Marekani
kwa ajili ya mkutano utakaofanyika kati ya tarehe 4 hadi 7 August 2014.
Safari hii ni kwa ajili ya shughuli za One Campaign ili kushiriki
kutoa mchango wa kuimarisha mazungumzo kati ya serikali ya Marekani na
nchi za Africa kwenye US-Africa Leaders Summit.
Rais Barack Obama atawakaribisha viongozi kutoka Africa kwenye
mkutano wa siku tatu ambapo kwenye safari hii, wasanii watakuwa pia na
mkutano na viongozi wa juu wa Marekani,wengine ni kutoka Young African
Leaders Initiative (YALI) na members of congress.
Kwenye mikutano hii wasanii kwa pamoja watafanya utetezi na
kusisitiza wananchi wa Africa kuchukua hatua za kujihusisha na kilimo
kama ONE campaign pia wasanii watafanya show kwa kuimba wimbo wa Cocoa
Na Chocolate.
List ya wasanii ni A.Y. (Tanzania), Buffalo Souljah (Zimbabwe),
D’Banj (Nigeria), Fally Ipupa (DRC), Femi Kuti (Nigeria), Judith Sephuma
(South Africa), Omawumi (Nigeria), Victoria Kimani (Kenya) na Wax Dey
(Cameroon).
Kwenye hii safari pia Ay amesindikizwa na mshkaji wake wa longtime Mwana FA.
No comments:
Post a Comment