PHIRI AKIWA MAZOEZINI NA AMRI KIEMBA |
Mohamed Selemani, Zanzibar
Phiri raia wa Zambia amewaambia viongozi kuwa
anataka ugumu wa timu wanazocheza nazo mechi za kirafiki uzidi kupanda ili kusaidia kukijenga kikosi hicho.
“Tunatafuta mechi ngumu zaidi kila baada ya
mechi moja, haya ni maelekezo ya Kocha Phiri.
“Hivyo mechi zitazidi kuwa ngumu zaidi
kuhakikisha tunajenga kikosi,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba kuhusiana na
uamuzi wa kocha huyo.
Tayari Simba imecheza mechi moja na kuitwanga
Kilimani kwa mabao 2-1.
Hata hivyo, Kilimani walionekana ni wepesi
kuliko Simba na Phiri akasisititiza, taratibu kikosi chake kitakwenda
kinafunguka.
No comments:
Post a Comment