Tuesday, 26 August 2014

RONALDO NA BENZEMA WOTE WAFUNGA REAL IKIIANZA LA LIGA KWA USHINDI WA 2-0 NYUMBANI

REAL Madrid jana imeuanza vyema msimu mpya wa La Liga kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cordoba iliyopanda daraja Uwanja wa Bernabeu. 
Shukurani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Mfaransa Karim Benzema dakika ya 30 na Mwanasoka Bora wa Dunia, Mreno Cristiano Ronaldo dakika ya 90.

Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Arbeloa/Carvajal dk73, Ramos, Pepe, Marcelo, Kroos, Modric, Bale, James/Isco dk72, Ronaldo na Benzema/Khedira dk76.
Cordoba: Carlos, Gunino, Inigo, Pantic, Crespo, Rossi, Garai, Pinillos/Cartabia dk46, Ryder/Fidel  dk62, Lopez Silva na Havenaar/Xisco dk67.

No comments:

Post a Comment