KOCHA
bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick
Phiri anatarajiwa kutua Dar es Salaam Ijumaa wiki hii kwa ajili ya
kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC.
Mzaliwa
huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na
Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio
makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi.
Mzambia
huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya
2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la
Tanzania na Kenya.Mazungumzo
yamekwishanyika na makubaliano yamefikiwa baina ya Phiri na Simba SC na
sasa atakuja kufanya kazi tena Msimbazi, akisaidiwa na Nahodha wake
enzi zake akifundisha timu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’.
Phiri
ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni
mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa
zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila
kufungwa hata mechi moja.
Lakini
pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi,
Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya
kipekee Msimbazi.
Katika
awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa-
kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.
Kwa
sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili,
Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green
Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.
Phiri
ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana
United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia
kama mshambuliaji.
Alikuwemo
kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za
Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo
kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana.
Akiwa
kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa
miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia
nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka
nchini mwake mwaka 1999.
Simba
SC jana ilivunja mkataba na Mcroatia, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku
moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika
mchezo wa kirafiki juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Loga
ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa
amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu na Rais wa
klabu hiyo, Evans Aveva alisema jana kwamba uamuzi huo umekuja baada ya
kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.
Loga
ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba
mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.
Loga
aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’,
aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini
mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam
FC mabingwa.
No comments:
Post a Comment