KOCHA Louis van Gaal amesema kwamba
kujiamini kwa Manchester United itaondoka
baada ya kipigo cha jana cha mabao 2-1 katika
mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England
nyumbani mbele ya Swansea.
Bao la Gylfi Sigurdsson dakika ya 72 lilimvuruga
kocha mpya wa United, Van Gaal kuftia ushindi
mfululizo katika mechi sita za kujiandaa na
msimu, Mashetani hao Wekundu wakifungwa
kwa mara ya kwanza nyumbani katika mchezo
wa ufunguzi ndani ya miaka 42.
"Unaposhinda kila kitu katika wakati wa
maandalizi na kuja kufungwa mechi ya kwanza,
hiyo haiwezi kuwa mbaya," amesema.
"Tumejijengea hali ya kujiamini kwa kiasi
kikubwa na kisha itaondoka kwa sababu ya
matokeo haya,".’
Mwanzo mbaya: Louis van Gaal akiondoka
uwanjani jana baada ya Manchester United
kuchapwa na Swansea
Mholanzi huyo alilazimika kuwachezesha kwa
mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya England
Jesse Lingard na Tyler Blackett, akiwa amesaini
wachezaji wawili tu wapya— Ander Herrera na
Luke Shaw msimu huu.
Alipoulizwa kama kipigo hicho kitamlazimu
kuingie sokoni kusajili kuboresha kikosi, Van Gaal
alisema: "Nilifikiri hivyo mkabla ya mechi hii,
hivyo hakuna tofauti. Wakati tunacheza
Marekani niliona kama hivyo. Kweli tunahitaji
mabeki. Lakini huwezi kusema hivyo, kwa
sababu tumepoteza mechi moja na tumeshinda
nyingine zote, hiyo ni beki. Ni timu ambavyo
tumecheza,".
Katika staili yake maarufu, Van Gaal, Mholanzi
hiyo hakumnyooshea kidole yeyote baada ya
mechi. Kocha huyo mpya wa United, aliwalaumu
wachezaji wake kwa kucheza ovyo. Pia alisema
walikosa hali ya kujiamini na hawakucheza
kitimu.
"Ni siku mbaya sana kwetu. Imewaangusha sana
wachezaji, mashabiki, mimi, na
viongozi,"alisema.
Saturday, 16 August 2014
VAN GAAL ASEMA KIPIGO CHA KIJANA KITAPOTEZA KUJIAMINI MAN UNITED, AKIRI PIA IPO HAJA YA KUSAJILI, HASWA MABEKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment