Saturday, 16 August 2014

ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, SPURS NAYO YAUA MTU

BAO la dakika ya 90 na ushei la Aaron Ramsey
limeipa mwanzo mzuri Arsenal katika Ligi Kuu ya
England, baada ya kuichapa 2-1 Crystal Palace
kwenye Uwanja wa Emirates, London.
Ilibaki kidogo tu Gunners kuanza kwa sare baada
ya Crystal kutangulia kupata bao kupitia kwa
Brede Hangeland dakika ya 35 kabla ya Laurent
Koscielny kuisawazishia Arsenal dakika ya 45 na
ushei.
Refa Jon Moss alimtoa nje kwa kadi ya pili ya
njano na kuwa nyekundu Jason Puncheon wa
Crystal Palace dakika ya 88 baada ya
kumchezea rafu Monreal.
Kikois cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Debuchy,
Chambers, Koscielny, Gibbs/Monreal dk53,
Wilshere/Oxlade-Chamberlain dk69, Arteta,
Sanchez, Ramsey, Cazorla, Sanogo/Giroud dk62.
Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann/Delaney
dk75, Hangeland, Ward, Puncheon, Jedinak,
Ledley, Bolasie/O'Keefe dk90, Chamakh na
Campbell/Gayle dk85.
Katika mechi nyingine za ufunguzi leo Ligi Kuu
England, Stoke City imelala nyumbani 1-0 mbele
ya Aston Villa, bao pekee la Andreas Weimann
dakika ya 50 Uwanja wa Britannia, Leicester City
imetoka sare ya 2- 2 na Everton, Queens Park
Rangers imefungwa 1-0 nyumbani na Hull City,
bao pekee la James Chester dakika ya 52
Uwanja wa Loftus Road,
West Bromwich Albion imetoka 2-2 na
Sunderland Uwanja wa The Hawthorns, West
Ham United imefungwa 1-0 nyumbani na
Tottenham Hotspur bao pekee la Eric Dier dakika
ya 90 na ushei Uwanja wa Boleyn Ground, wakati
Manchester United imefungwa 2-1 nyumbani na
Swansea City.

No comments:

Post a Comment