Alisema mbali Diamond na Twanga Pepeta pia wasanii wengine wa kizazi kipya kama Dully Sykes, Barnaba, Mataluma pamoja na makundi ya kudansi watajumuika katika onyesho hilo. Alisema mbali na burudani hizo, kutakuwa na mechi za vijana kati ya under 20 za Simba na Azam, Simba kubwa ikipambana na Zesco United ya Zambia. Kaburu alisema kiingili katika tamasha hilo shilingi 5000/=, kwa majukwaa ya kijani, bluu na orange huku VIP itakua ni shilingi 20000/=. Katika hatua nyingine, Simba imeahidi kushusha jeshi kamili katika mechi yao ya kirafiki na Zesco ya Zambia itakayofanyika kesho katika Uwanja wa Taifa. Mechi hiyo itakuwa ni maalum kwa ajili ya kusherekea tamasha la Simba Day linalofanyika kila mwaka na Kaburu amesema wachezaji wote waliosajili msimu huu wataonekana katika mechi hiyo muhimu. “Wachezaji wao wote wapya watawaanika siku hiyo ambapo tayari hata mshambuliaji wetu mpya Paul Kiongere ameshawasili nchini kwa ajili ya kuonekana katika siku hiyo,”alisema. Naye Meneja wa Zesco, Mavuto Banda alisema mashabiki wa timu hiyo wajumuike katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuona burudani ambayo wameiandaa.
“Siwezi kusema tutawafunga magoli mangapi lakini ni lazima tutawafunga kwani nasi tunataka kuonyesha makali ya kikosi chetu siku hiyo na wataona sherehe hizo chungu,” alisema.
No comments:
Post a Comment