Kocha Mkuu mpya wa Simba, Mzambia,
Patrick Phiri, ameshtushwa na taarifa za kipa wake, Juma Kaseja na beki wa kati
Kelvin Yondani, kuichezea Yanga huku akitamka kuwa wataonana uwanjani.
Phiri alisema kuwa ni ngumu kuwazuia wachezaji kwenda kuichezea timu hiyo, yote
ni katika kutafuta maisha.
Phiri alisema, kikubwa anawatakiwa
kila la kheri wachezaji hao huku akiwataarifu wataonana uwanjani mara timu hizo
zipokutana kwenye ligi na mashindano mengine.
“Ni maendeleo mchezaji anapotoka
kwenda sehemu nyingine, lakini kwangu ninashangaa Kaseja na Yondani kwenda
kuichezea timu pinzani.
“Ninaamini wachezaji hao wamefuata
maslahi mazuri waliyoahidiwa Yanga katika kutafuta maisha, lakini kikubwa
ninawatakia maisha mema huko walipo,” alisema Phiri aliyewahi kuwafundisha
wachezaji hao wakiwa wanaichezea Simba.
No comments:
Post a Comment