Monday, 4 August 2014

VAN GAAL AREJESHA FURAHA MAN UNITED, YAWAFUMUA LIVERPOOL 3-1 NA KUBEBA MWALI WA KIMATAIFA MAREKANI

LOUIS Van Gaal ametwaa taji la kwanza Manchester United baada ya usiku wa kuamkia leo kuwachapa mahasimu, Liverpool mabao 3-1 Uwanja wa Sun Life mjini Miami, Marekani na kubeba Kombe la Kimataifa, michuano ya klabu kujiandaa na msimu mpya.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Rooney dakika ya 55, Mata 57 na Lingard 88, baada ya Gerrard kutangulia kuwafungia Liverpool kwa penalti dakika ya 14.
Kikosi cha Man United kilikuwa; De Gea, Evans/Blackett dk46, Smalling, Jones, Valencia/Shaw dk9, Herrera/Lingard dk78, Fletcher/Cleverley dk46, Young, Mata/Kagawa dk68, Rooney na Hernandez/Nani dk68.
Liverpool; Mignolet, Kelly, Johnson, Skrtel, Sakho/Toure dk74, Gerrard/Lucas dk62, Allen/Ibe dk62, Henderson, Coutinho/Peterson dk77, Lambert/Can dk62 na Sterling.

No comments:

Post a Comment