Monday, 25 August 2014

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA..DIMARIA UYOO MAN U

Manchester United wamekamilisha majadiliano
na Real Madrid na watalipa pauni milioni 63.9
na kuvunja rekodi ya Uingereza kumnunua
winga Angel Di Maria (Sky Sports), mchezaji
huyo kutoka Argentina huenda akafikia kuuzwa
kwa pauni milioni 72, milioni 60 zikilipwa
mwanzo na milioni 12 baadaye (Daily Mirror),
Juventus wataanza mazungumzo na Arsenal
kuhusu Lukas Podolski. Juventus wanamtaka
kwa mkopo lakini Arsenal wanataka kumuuza
(Daily Telegraph), boss wa Real Madrid Carlo
Ancelotti amesema Sami Khedira, 27,
hatoondoka licha ya kufuatiliwa na Arsenal,
Bayern Munich na Manchester United
(Guardian), meneja wa Everton Roberto
Martinez amesema bado anaweza kumsajili
Samuel Eto'o, 33, au Danny Welbeck, 23, katika
wiki ya mwisho ya dirisha la usajili (Times),
boss wa Arsenal Arsene Wenger amemuulizia
beki mkabaji wa Brazil Luiz Gustavo, 27,
anayechezea Wolfsburg (Daily Mirror),
Southampton wamepanda dau kwa winga wa
Tottenham Andros Townsend, 23, (ESPN FC),
meneja wa Southampton Ronald Koeman yuko
tayari kuanza kumfuatilia tena winga wa
Norwich Nathan Redmond, 20, (Sun), Liverpool
watalazimika kuchukua hatua za haraka
kumsajili Radamel Falcao, 28, wakati Juventus
wakimtaka mshambuliaji huyo wa Monaco kwa
mkopo (Daily Star), Fernando Torres
hatoondoka Chelsea bila ya mkataba wa kitita
cha pauni milioni 8.5 kutolewa. Roma
wanamtaka mshambuliaji huyo (Sun),
Sunderland wamekuwa na mazungumzo na
winga wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou,
29, ambaye pia anatazamwa na Arsenal,
Liverpool na Everton (Daily Express), boss wa
Sunderland ana matumaini ya kupata jibu
iwapo mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini,
23, atajiunga nao au la (Sunderland Echo), West
Ham wamemuulizia beki wa Manchester City
Micah Richards, 26, ambaye anaonekana
huenda akaondoka City wiki hii (Sun), QPR
wamehusishwa na kipa wa Reading Alex
McCarthy, 24, (Daily Star), AC Milan
wanamtaka Samuel Eto'o na Fernando Torres
kuziba pengo la Mario Balotelli (Gazetta dello
Sport), Juventus wana nafasi kubwa ya
kumshawishi Radamel Falcao kujiunga nao kwa
mkopo wa mwaka mmoja (Gazetta dello Sport),
Lukas Podolski huenda akasaini mkataba wa
miaka mitatu na Wolfsburg na watalipa euro
milioni 12 kumsajili kutoka Arsenal (L'Equipe).
Zimesalia siku saba kabla ya dirisha la usajili
kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Cheers!!!!

No comments:

Post a Comment