Tuesday, 7 October 2014

MAHAKAMA HUENDA IKAZUIA KUFANYIKA KWA MISS TANZANIA 2014

MWANZILISHI wa mashindano ya urembo ya
Miss Tanzania , Prashant Patel , amefungua
maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam akiomba mshirika
wake, Hashim Ludenga , azuiliwe kuendelea
kuendesha mashindano hayo yanayotarajiwa
kufikia kilele chake Oktoba 11, mwaka huu.
Patel amewasilisha maombi hayo katika hati
ya dharura kupitia wakili wake, Benjamin
Mwakagamba , akidai Lundenga ana mpango
wa kuendesha mashindano hayo kwenye
Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam,
kinyume cha sheria na bila hata kumtaarifu.
Anaomba mahakama itoe zuio dhidi ya
Lundenga , la kuendesha mashindano hayo
hadi shauri lake la msingi aliloliwasilisha
litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi . Katika
kesi yake ya msingi, Patel anadai pamoja na
mambo mengine, utekelezaji wa makubaliano
ya Februari 20 , 2012 na malipo ya Sh milioni
19 ambayo hayajalipwa kwa mujibu wa
mkataba na faida nyinginezo ambazo
zimejitokeza hadi Septemba 23, mwaka huu.
Shauli hilo limepangwa kutajwa mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi Frank Moshi leo ,
na Lundenga ametakiwa kuwasilisha utetezi
wake ndani ya siku 21 , na akishindwa
kufanya hivyo , mahakama itaendelea kutoa
hukumu dhidi yake. Katika hati ya kiapo
inayounga mkono maombi yake , Patel anadai
kuwa yeye pamoja na Lundenga ndio
waanzilishi, waongozaji na waendeshaji wa
mashindano ya Miss Tanzania na wamekuwa
katika hali hiyo kwa miaka 20 sasa , tangu
mashindano hayo yaliyoporuhusiwa tena
mwaka 1994 . Kwa kipindi chote hicho,
wamekuwa wakisaini makubaliano ya namna
ya kuendesha mashindano hayo na mara ya
mwisho walisaini makubaliano Februari 20,
2012. Hata hivyo , Lundenga alikataa kusaini
makubaliano kwa mwaka 2013 na 2014 na
ameshindwa kumlipa fedha zake Sh milioni
19. Patel anadai badala yake Ludenga
ameshirikiana na wadhamini wengine
kuendesha mashindano hayo. Kwa mujibu wa
makubaliano , Lundenga pia alipaswa kulipa
pauni za Uingereza 30, 000 kama malipo ya
kibali kwa mwendeshaji wa shindano hilo
duniani, Miss World, deni ambalo limekuwa la
muda mrefu, hivyo kuchafua hadhi yake .
Patel anadai kuwa Ludenga alipelekewa
taarifa na wakili wake kulimaliza suala hili
bila kushirikisha hatua za kisheria , lakini
alikaidi na kukataa . Hivyo Patel anadai kuwa
hakuwa na njia nyingine zaidi ya kulipeleka
suala hilo mahakamani

Kumekucha : Maalim Seif Hamad Kujiuzulu Umakamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar...

Hali ya mambo visiwani Zanzibar siyo nzuri
hata kidogo, (wala si ya kufurahia) toka jana
jioni ilipotoka taarifa ya kufukuzwa kazi kwa
Mwanasheria Mkuu wa SUK Athuman Masoud.
Kumekuwa na vikao usiku kucha kwa viongozi
na wanachama wa CUF Zanzibar, na kuazimia
pamoja na mambo mengine kufanya tathimini
ya "KUJIUZULU" kwa makamo wa kwanza wa
rais wa serikali ya umoja wa kitaifa. Maalim
Seif.
Naam, mmoja wa vijana aliepewa kazi ya
kupima upepo ambaye ni mwanasheria wa
CUF, anaangalia swala hili kisheria
(ikumbukwe kuna makubaliano ya kisheria
katika kuongoza SUK).
Baadhi wamepewa angles tofauti na kutoa
majibu mapema iwezekanavyo.
Ili Mheshimiwa achukue uamuzi Mgumu
haraka leo.
Kama ikiwa ndio hivyo, kesho Media zote ni
kujiuzulu kwa Sharif na si kupokeaji wa katiba.
My take:
Kama karidhia yeye mwenyewe Mh.Maalim, na
iwe hivyo ila kama ni kupata attention ya
media tu siyo.

Viboko vyatembezwa makaburini Sengerema

Wajukuu wa marehemu Sabina Ngalu wa
Mwanza wamecharazwa viboko na watoto wa
marehemu baada ya kung’ang’ania kaburini
wakitaka wapewe fedha.
Chanzo cha wajukuu hao zaidi ya 10
kucharazwa bakora ni kung’ang’ania ndani ya
kaburi lililokua limeandaliwa kwa ajili ya
kuhifadhi mwili wa marehemu wakitaka
wapewe ng’ombe mmoja au sh.100,000 kama
zinavyotaka mila za kabila la kisukuma.
Gazeti la MTANZANIA ambalo lilikua shuhuda
katika eneo hilo lilisema kitendo hicho kilimkera
Padri Nicodemus Mayalla aliyekua akiendesha
ibada eneo hilo huku akiwataarifu polisi kuhusu
vurugu hizo hata hivyo kaka mkubwa wa
marehemu aliamua kuchukua fimbo na kuanza
kuwachapa.
Kitendo cha kuwachapa kiliamsha hasira zaidi
kwa wajukuu hao ambao nao walijibu kwa
kurusha michanga wakiwa ndani ya kaburi hadi
waombolezaji walipoamua kuchanga na
kuwapa fedha hizo ndipo walipotoka.
Hata hivyo Padri huyo aligoma kurejea eneo la
makaburi kuongoza ibada hadi hapo watoto
hao watakaporudisha fedha hizo na kuomba
radhi,jambo ambalo lilitekelezeka.

BARCELONA KUTIMULIWA LA LIGA IWAPO KATALUNYA ITAJITENGA HISPANIA

KLABU ya Barcelona haitaruhusiwa kucheza
La Liga ikiwa Katulonya itajitenga kutoka
Hispania, Mkuu wa ligi ya nchi hiyo, Javier
Tebas amesema hayo juu ya uwezekano wa
mgawanyiko wa taifa hilo mwezi ujao.
Tebas amefafanua kwamba sheria za
michezo za nchi hiyo zinaruhusu nchi moja
tu ambayo si sehemu ya Hispania - Andorra
- kushiriki ligi hiyo au mashindano mengine,
na FC Andorra tayari inacheza katika mfumo
wa za Hispania.
Huku La Liga tayari ikionekana kuwa na
timu mbili zinazochuana vikali kwenye vita
ya mataji (pamoja na Atletico Madrid
kushinda taji msimu uliopita kuzima utawala
wa Real na Barca kwa misimu tisa)
kuwapoteza vigogo hao wa Katalunya
litakuwa pigo kubwa kwa soka ya Hispania.
Vigogo wa Hispania, Barcelona moja kwa
moja watakuwa wamejiondoa La Liga ikiwa
Katalunya litakuwa taifa huru
"Ikiwa Katalunya litakuwa taifa huru, kwa
kuzingatia Sheria za Michezo Hispania,
kwamba Barcelona haitaruhusiwa kucheza,"
Tebas, rais wa LFP, amewaambia Waandishi
wa Habari mjini Barcelona.
"Yatahitajika mabadilika katika sheri a
zilizowekwa na Bunge la Hispania. Wazi,
iwapo itatokea litakuwa pigo kubwa katika
soka ya Hispania kuwap[oteza Barca.
"Sipati picha LFP bila Barca. Kwa namna
hiyo hiyo siwezi kupata picha Katalunya bila
Hispania, Siioni La Liga bila Barca. Pia ikiwa
itatokea hivyo, utaiitaje hiyo ligi: Ligi ya
Hispania au Ligi ya Iberia?'
Sababu ambazo zimeipa Andorra fursa ya
kucheza ligi ya Hispania, nchi ndogo
kwenye milima ya Pyrenees
inayozitenganisha Hispania na Ufaransa-
zinaweza kutumika pia kuzifanya klabu za
Katalunya ziendelee kushiriki.
Barcelona, ikiwa na nyota kama Lionel Messi
katika timu yao, watabaki kucheza Ligi ya
Katalunya
Xavi na Gerard Pique ni miongoni mwa
wachezaji wa Barca waliojitokeza
kuunga mkono kung a mkono kujitenga kwa
Katalunya. Serikali ya Katalunya itaamua
Oktoba 15 juu ya mustakabali wa nchi yao.

Thursday, 4 September 2014

MARCOS ROJO APATIWA KIBALI CHA KUPIGA MZIGO MAN UNITED, VAN GAAL SASA ROHO KWATUUU

BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo
anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza klabu
yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England
dhidi ya Queens Park Rangers Uwanja wa Old
Trafford Septemba 14 baada ya kupatiwa hati ya
kufanya kazi.
Rojo alisafiri hadi Lisbon Alhamisi ili kukamilisha
taratibu za kupata hati hiyo ya kufanyia kazi
England.
Kufanikiwa kwa mchezaji huyo kupata hati hiyo
ya kufanyia kazi ni faraja kwa kocha Louis van
Gaal, ambaye kikosi chake mina tatizo la safu ya
ulinzi.
Uthibitisho: Marcos Rojo amepatiwa hati ya
kufanyia kazi maana yake sasa anaweza
kuichezea Manchester United kwa mara ya
kwanza dhidi ya QPR

RONALDO AFUNGUA MTIMA WAKE; "MAN UNITED IPO MOYONI MWANGU, NATAMANI

MWANASOKA Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo
amesema kwamba Manchester United ni klabu
ambayo ipo moyoni make na anatamani siku
moja are jee kucheza tena.
Mchezaji huyo wa Real Madrid na Ureno
ameweka wazi "MaipendaI Manchester," na
kuongeza;
"Kila mmoja anajua hilo — nimesema hivyo mara
nyingi. Manchester ipo moyoni mwangu.
Nimeacha marafi wengi huko, mashabiki
wanavutia sana na ninatamani siku moja
ningerudi,".

Monday, 1 September 2014

KWA MZIKI HUU BADO MANCHESTER UNITED ITASHINDWA KUINUKA KWELI?


KINAVYOTARAJIWA KUPANGWA KIKOSI CHA MANCHESTER UNITED BAADA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA NA YENYEWE IKIWA NA WACHEZAJI WAPYA KIBAO. KWA KIKOSI UNACHOKIONA, KWELI ITASHINDWA KURUDISHA ILE HESHIMA YAKE? ITAKUWA KASHESHE.

DIRISHA LA USAJILI LAFUNGWA; WALIOTOKA NA KUINGIA KLABU ZOTE ENGLAND HADI SEKUNDE YA MWISHO WAKO HAPA

Mtu wa kazi; Radamel Falcao amehamia Manchester United kwa mkopo kutoka Monaco ya Ufaransa
DIRISHA la usajili limefungwa usiku wa kuamkia leo na klabu mbalimbali zilikuwa kwenye pilika za kukamilisha uhamisho wa nyota mbalimbali waliokuwa wakiwahitaji.
  KITOMIXNEWS inakuletea orodha ya wachezaji wote wapya waliosajiliwa pamoja na wale ambao wameondoka kwenye klabu zao baada ya kufungwa kwa usajili mkubwa wa majira haya.

VAN GAAL AHAMIA KWENYE UKUTA, AMNASA BEKI BORA WA UHOLANZI KUTOKA AJAX



 Unaweza kudhani Louis van Gaal amelala na anasajili washambuliaji tu, la! Wakati dirisha la usajili linakwenda ukingoni kufungwa, Manchester United imemnasa beki kisiki wa Ajax, Daley Blind.

WELBECK AENDA KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA ARSENAL....FALCAO ACHUKUA NAFASI YAKE OLD T.

KLABU ya Arsenal inapambaa dakika za
mwishoni kuelekea kufungwa dirisha la usajili
kuhakikisha inakamilisha uhamisho wa
mshambuliaji wa Manchester United, Danny
Welbeck kwa dau la Pauni Milioni 6.
Hiyo inafuatia The Gunners kumkosa
mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao,
ambaye amehamia Manchester United leo.
Hivi sasa inaelezwa Welbeck anafanyiwa vipimo
vya afya Arsenal kukamilisha uhamisho huo.

CHICHARITO AFAULU VIPIMO VYA AFYA, RASMI NI MCHEZAJI WA REAL MADRID

MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amekamilisha
uhamisho wake wa mkopo kwenda Real Madrid
pamoja na uwezekano wa kununuliwa moja kwa
moja kutoka Manchester United baadaye.
Real inamchukua mchezaji huyo baada ya
kufaulu vipimo vya afya leo mjini Madrid.
United inataka dau la Pauni Milioni 17 kumuuza
moja kwa moja mchezaji huyo, lakini kwa
mkataba wa sasa wa mkopo wa muda mrefu wa
msimu, Louis van Gaal anachukua Pauni Milioni
1.5.
United imethibitisha katika ukurasa wake wa
Twitter leo kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo
kwenda Real Madrid.

Friday, 29 August 2014

RONALDO ALIVYOSHEREHEKEA TUZO YAKE YA UFALME WA SOKA ULAYA LEO UFARANSA


Busu kwenye tuzo: Nyota wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo akibusu tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Ulaya baada ya kukabidhiwa usiku wa leo mjini Monaco, Ufaransa

Tuesday, 26 August 2014

PHIRI ATAKA UGUMU WA MECHI SIMBA UENDE UNAONGEZEKA


PHIRI AKIWA MAZOEZINI NA AMRI KIEMBA

Mohamed Selemani, Zanzibar
Kocha Patrick Phiri wa Simba, ametaka kikosi chake kuongezewa mechi ngumu.

BARUA YA DI MARIA YAWAACHA NA MAJONZI WACHEZAJI, MASHABIKI WA REAL MADRID




Kiungo mshambuliaji mpya wa Manchester United, Angel Di Maria ameandika barua iliyowasikitisha wachezaji na mashabiki wa Real Madrid.

GIGGS AANGUA KILIO BENCHI ,,,,MAN UNITED IKIPIGWA 4-0 NA KITIMU CHA 'MCHANGANI' USKU HUU

Analia: Kocha Msaidizi Ryan Giggs akiwa ameshika kichwa akilia kwa uchungu mwishoni mwa mchezo huo, huku kocha Louis van Gaal akiwa haamini macho yake
 KOCHA Louis van Gaal ameendelea kuogelea katika bwawa la maji moto Manchester United, baada ya usiku huu kfungwa na Mk Dons ya Daraja la Kwanza mabao 4-0 katika michuano ya Kombe la Ligi, maarufu Capital One.

DI MARIA ASAINI MAN UNITED, VAN GAAL AMKABIDHI JEZI YEYE MWENYEWE


Tumempata! Angel di Maria akikabidhiwa jezi ya Manchester United na kocha wa Louis van Gaal
 HATIMAYE Angel di Maria amekuwa mchezaji wa Manchester United kwa dau la rekodi Uingereza la Pauni Milioni 59.7 usiku huu kutoka Real Madrid.

KIBALI CHAMKWAMISHA BEKI MPYA KUANZA KAZI MAN UNITED

Subiri kijana: Marcos Rojo (kulia) hatakuwepo katika mchezo dhidi ya MK Dons kwa sababu ya kibali cha kufanyia kazi Uingereza

BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo hatacheza leo dhidi ya MK Dons kutokana na kwamba bado hajapata kigali cha kufanyia kazi nchini Uingereza.

Wanajeshi wa Urusi walikuwa Ukraine kimakosa


Baadhi ya watu kumi waliokamatwa na jeshi la Ukraine
Urusi imesema kwamba kikundi cha wanajeshi wa Urusi ambacho kimekamatwa mashariki mwa Ukraine kilikuwa kimevuka mpaka huo kimakosa huku Ukraine ikisema kwamba wanajeshi 10 walikuwa wamekamatwa.

RONALDO NA BENZEMA WOTE WAFUNGA REAL IKIIANZA LA LIGA KWA USHINDI WA 2-0 NYUMBANI

REAL Madrid jana imeuanza vyema msimu mpya wa La Liga kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cordoba iliyopanda daraja Uwanja wa Bernabeu. 

Monday, 25 August 2014

SURE BOY AREJESHWA KIKOSINI

KIUNGO wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure
Boy’ amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akiitwa
kwa mara ya kwanza chini ya kocha Mholanzi,
Mart Nooij.
Nooij ametaja kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili
ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya
Morocco utakaochezwa Septemba 5, mwaka huu
nchini Morocco.
Wachezaji wengine wapya katika kikosi hicho
kutoka kile kilichotolewa na Msumbiji katika
mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika
ni kiungo Said Ndemla wa Simba SC na
washambuliaji Mwagane Yeya wa Mbeya City na
Juma Luizio wa ZESCO United ya Zambia.
Kikosi kamili ni makipa; Deogratias Munishi
(Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said
Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari
Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin
Yondani (Azam), Aggrey Morris (Azam), Joram
Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto
(Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba),
Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam),
Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na
Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis
Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana
Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa
(Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma
Liuzio ZESCO, Zambia).
Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini
Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika
hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na
kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam.

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA..DIMARIA UYOO MAN U

Manchester United wamekamilisha majadiliano
na Real Madrid na watalipa pauni milioni 63.9
na kuvunja rekodi ya Uingereza kumnunua
winga Angel Di Maria (Sky Sports), mchezaji
huyo kutoka Argentina huenda akafikia kuuzwa
kwa pauni milioni 72, milioni 60 zikilipwa
mwanzo na milioni 12 baadaye (Daily Mirror),
Juventus wataanza mazungumzo na Arsenal
kuhusu Lukas Podolski. Juventus wanamtaka
kwa mkopo lakini Arsenal wanataka kumuuza
(Daily Telegraph), boss wa Real Madrid Carlo
Ancelotti amesema Sami Khedira, 27,
hatoondoka licha ya kufuatiliwa na Arsenal,
Bayern Munich na Manchester United
(Guardian), meneja wa Everton Roberto
Martinez amesema bado anaweza kumsajili
Samuel Eto'o, 33, au Danny Welbeck, 23, katika
wiki ya mwisho ya dirisha la usajili (Times),
boss wa Arsenal Arsene Wenger amemuulizia
beki mkabaji wa Brazil Luiz Gustavo, 27,
anayechezea Wolfsburg (Daily Mirror),
Southampton wamepanda dau kwa winga wa
Tottenham Andros Townsend, 23, (ESPN FC),
meneja wa Southampton Ronald Koeman yuko
tayari kuanza kumfuatilia tena winga wa
Norwich Nathan Redmond, 20, (Sun), Liverpool
watalazimika kuchukua hatua za haraka
kumsajili Radamel Falcao, 28, wakati Juventus
wakimtaka mshambuliaji huyo wa Monaco kwa
mkopo (Daily Star), Fernando Torres
hatoondoka Chelsea bila ya mkataba wa kitita
cha pauni milioni 8.5 kutolewa. Roma
wanamtaka mshambuliaji huyo (Sun),
Sunderland wamekuwa na mazungumzo na
winga wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou,
29, ambaye pia anatazamwa na Arsenal,
Liverpool na Everton (Daily Express), boss wa
Sunderland ana matumaini ya kupata jibu
iwapo mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini,
23, atajiunga nao au la (Sunderland Echo), West
Ham wamemuulizia beki wa Manchester City
Micah Richards, 26, ambaye anaonekana
huenda akaondoka City wiki hii (Sun), QPR
wamehusishwa na kipa wa Reading Alex
McCarthy, 24, (Daily Star), AC Milan
wanamtaka Samuel Eto'o na Fernando Torres
kuziba pengo la Mario Balotelli (Gazetta dello
Sport), Juventus wana nafasi kubwa ya
kumshawishi Radamel Falcao kujiunga nao kwa
mkopo wa mwaka mmoja (Gazetta dello Sport),
Lukas Podolski huenda akasaini mkataba wa
miaka mitatu na Wolfsburg na watalipa euro
milioni 12 kumsajili kutoka Arsenal (L'Equipe).
Zimesalia siku saba kabla ya dirisha la usajili
kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Cheers!!!!

TANZANIA KUANDAA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA BAADA YA LIBYA KUJITOA

TANZANIA itaomba kuandaa Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017, kufuatia
Libya kujitoa.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ameiambia KITOMIXNEWS leo
kwamba wana uwezo na wako tayari kuwa
wenyeji wa fainali hizo- hivyo wataomba.
“Tutaomba kuwa wenyeji wa AFCON ya 2017
kuziba pengo la Libya, tuko tayari na tuna
uwezo, tunatarajia sapoti kubwa ya Serikali na
wadau wengine wa Tanzania katika
hili,”amesema Malinzi.
Libya imeamua kujitoa kutokana na vurugu za
kisiasa zinazoendelea nchini humo- hivyo
kuhofia mazingira ya kiusalama.
Awali, Libya ilipewa uenyeji wa fainali za mwaka
2013, lakini ikajitoa kwa sababu kama hizo na
Afrika Kusini ikapewa nafasi hiyo- huku
makubaliano yakifikiwa wao wataandaa AFCON
ya mwaka 2017.
Jumamosi ikatangazwa tena, Libya imejitoa
baada ya viongozi wa nchi hiyo kukutana na
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa
Hayatou.
CAF ikasema jitihada za kumsaka mbadala wa
Libya zinaanza mara moja- maana yake
kujitokeza kwa Tanzania ni ahueni kwao.
Kwa sasa, Tanzania inaweza kabisa kuwa
mwenyeji wa fainali hizo kwa kuwa ina viwanja
visivyopugua vitatu vyenye sifa, ingawa vingine
vitahitaji marekebisho madogo.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hakuna shaka
una sifa zote, wakati CCM Kirumba mjini
Mwanza na Sheikh Amri Abeid Arusha vitahitaji
marakebisho kidogo.
Iwapo Tanzania itafanikiwa kupata uenyeji wa
fainali za mwaka 2017, itakuwa imefuzu moja
kwa moja kucheza michuano hiyo bila kupitia
kwenye hatua ya mchujo.
Na hiyo itakuwa mara ya pili kihistoria kushiriki
AFCON baada ya 1980 mjini Lagos, Nigeria
wakati huo bado michuano hiyo ikiitwa Kombe la
Mataifa ya huru ya Afrika.
Tanzania ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji
Nigeria, Ivory Coast na Misri na ikashika mkia.
Ilifungwa 3-0 na Ngeria, 2-1 na Misri na kutoka
sare ya 1-1 na Ivory Coast.
Yapo matumaini makubwa Tanzania ikafanikiwa
kupewa yenyeji wa michuano hiyo mwaka 2017,
kutokana na uhusiano mzuri baina ya Hayatou
na rais wa sasa wa TFF, Malinzi. Kwa ujumla,
FIFA na CAF zina imani kubwa na utawala wa
Malinzi.

Wednesday, 20 August 2014

PHIRI AWAKUMBUKA KASEJA, YONDANI AKIWA ZANZIBAR


Kocha Mkuu mpya wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, ameshtushwa na taarifa za kipa wake, Juma Kaseja na beki wa kati Kelvin Yondani, kuichezea Yanga huku akitamka kuwa wataonana uwanjani.
Mzambia huyo alitua nchini wiki iliyopita kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na Ligi Kuu Bara iliyopanga kuanza Septemba 20, mwaka huu huku akisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha Simba.

ROJO ATUA MAN UNITED KUKAMILISHA USAJILI

KLABU ya Manchester United imekubali kutoa Pauni Milioni 16 kumnunua beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo.
Rojo, ambaye ametua mjini Manchester leo na kusema kuhamia United ‘anahisi kama ndoto’, anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka minne akifaulu vipimo vya afya na kukubali vipengele binafsi vya kandarasi yake.

JULIO CESAR ATUA BENFICA MIAKA MIWILI BAADA YA KUPOTEZA NAMBA QPR

KLABU ya Benfica imekamilisha usajili wa kipa wa kimataifa wa Brazil, Julio Cesar kwa mkataba wa miaka miwili kutoka QPR.
Mlinda mlango huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na klabu hiyo ya London mwaka 2012, lakini akacheza mechi 24 kabla ya kwenda kwa mkopo Toronto.

Saturday, 16 August 2014

ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, SPURS NAYO YAUA MTU

BAO la dakika ya 90 na ushei la Aaron Ramsey
limeipa mwanzo mzuri Arsenal katika Ligi Kuu ya
England, baada ya kuichapa 2-1 Crystal Palace
kwenye Uwanja wa Emirates, London.
Ilibaki kidogo tu Gunners kuanza kwa sare baada
ya Crystal kutangulia kupata bao kupitia kwa
Brede Hangeland dakika ya 35 kabla ya Laurent
Koscielny kuisawazishia Arsenal dakika ya 45 na
ushei.
Refa Jon Moss alimtoa nje kwa kadi ya pili ya
njano na kuwa nyekundu Jason Puncheon wa
Crystal Palace dakika ya 88 baada ya
kumchezea rafu Monreal.
Kikois cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Debuchy,
Chambers, Koscielny, Gibbs/Monreal dk53,
Wilshere/Oxlade-Chamberlain dk69, Arteta,
Sanchez, Ramsey, Cazorla, Sanogo/Giroud dk62.
Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann/Delaney
dk75, Hangeland, Ward, Puncheon, Jedinak,
Ledley, Bolasie/O'Keefe dk90, Chamakh na
Campbell/Gayle dk85.
Katika mechi nyingine za ufunguzi leo Ligi Kuu
England, Stoke City imelala nyumbani 1-0 mbele
ya Aston Villa, bao pekee la Andreas Weimann
dakika ya 50 Uwanja wa Britannia, Leicester City
imetoka sare ya 2- 2 na Everton, Queens Park
Rangers imefungwa 1-0 nyumbani na Hull City,
bao pekee la James Chester dakika ya 52
Uwanja wa Loftus Road,
West Bromwich Albion imetoka 2-2 na
Sunderland Uwanja wa The Hawthorns, West
Ham United imefungwa 1-0 nyumbani na
Tottenham Hotspur bao pekee la Eric Dier dakika
ya 90 na ushei Uwanja wa Boleyn Ground, wakati
Manchester United imefungwa 2-1 nyumbani na
Swansea City.

VAN GAAL ASEMA KIPIGO CHA KIJANA KITAPOTEZA KUJIAMINI MAN UNITED, AKIRI PIA IPO HAJA YA KUSAJILI, HASWA MABEKI

KOCHA Louis van Gaal amesema kwamba
kujiamini kwa Manchester United itaondoka
baada ya kipigo cha jana cha mabao 2-1 katika
mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England
nyumbani mbele ya Swansea.
Bao la Gylfi Sigurdsson dakika ya 72 lilimvuruga
kocha mpya wa United, Van Gaal kuftia ushindi
mfululizo katika mechi sita za kujiandaa na
msimu, Mashetani hao Wekundu wakifungwa
kwa mara ya kwanza nyumbani katika mchezo
wa ufunguzi ndani ya miaka 42.
"Unaposhinda kila kitu katika wakati wa
maandalizi na kuja kufungwa mechi ya kwanza,
hiyo haiwezi kuwa mbaya," amesema.
"Tumejijengea hali ya kujiamini kwa kiasi
kikubwa na kisha itaondoka kwa sababu ya
matokeo haya,".’
Mwanzo mbaya: Louis van Gaal akiondoka
uwanjani jana baada ya Manchester United
kuchapwa na Swansea
Mholanzi huyo alilazimika kuwachezesha kwa
mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya England
Jesse Lingard na Tyler Blackett, akiwa amesaini
wachezaji wawili tu wapya— Ander Herrera na
Luke Shaw msimu huu.
Alipoulizwa kama kipigo hicho kitamlazimu
kuingie sokoni kusajili kuboresha kikosi, Van Gaal
alisema: "Nilifikiri hivyo mkabla ya mechi hii,
hivyo hakuna tofauti. Wakati tunacheza
Marekani niliona kama hivyo. Kweli tunahitaji
mabeki. Lakini huwezi kusema hivyo, kwa
sababu tumepoteza mechi moja na tumeshinda
nyingine zote, hiyo ni beki. Ni timu ambavyo
tumecheza,".
Katika staili yake maarufu, Van Gaal, Mholanzi
hiyo hakumnyooshea kidole yeyote baada ya
mechi. Kocha huyo mpya wa United, aliwalaumu
wachezaji wake kwa kucheza ovyo. Pia alisema
walikosa hali ya kujiamini na hawakucheza
kitimu.
"Ni siku mbaya sana kwetu. Imewaangusha sana
wachezaji, mashabiki, mimi, na
viongozi,"alisema.

LIGI KUU ENGLAND YAANZA LEO, MAN UNITED YA VAN GAAL, CHELSEA YA MOURINHO YENYE DIEGO COSTA, LIVERPOOL BILA SUAREZ, ARSENAL MPYA NA MABINGWA MAN CITY…PATAMU HAPOO!

LIGI KUU ya England inaanza leo na Louis van
Gaal anaanzisha rasmi zama mpya Manchester
United atakapoiongoza dhidi ya Swansea City
Uwanja wa Old Traffford.
Mwalimu huyo wa Kiholanzi mwenye umri wa
miaka 63 amefanya vizuri katika wiki zake nne
za kwanza United, akiiwezesha timu kushinda
mechi tano na sare moja katika mech za
kujiandaa na msimu na sasa watu wanataka
kuangalia mafanikio yake katika ligi.
Swansea ni moja kati ya timu nane ambazo
msimu uliopita zilishinda mechi Old Trafford
Mashetani Wekundu wakiwa chini ya kocha
David Moyes aliyetupiwa virago kwa matokeo
mabaya mwishoni mwa msimu.
Ikumbukwe, United pia ilikutana na Swansea
katika mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu huo
2013-2014 wakiwa mabingwa watetezi na
kushinda mabao 4-1 Uwanja wa Liberty, siku za
mwanzoni za Moyes kazini.
Matokeo hayo hayakuwa na maana, kwani
mwishoni mwa msimu United ilimaliza katika
nafasi ya saba.
Wayne Rooney ataiongoza United kwa mara ya
kwanza tangu achaguliwe kuwa Nahodha
Jumanne timu hiyo ikishinda mabao 2-1 katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya Valencia.
United itamkosa beki wake kinda wa kushoto
mwenye umri wa miaka 19 iliyemnunua kwa
Pauni Milioni 27, Luke Shaw, ambaye
anasumbuliwa na maumivu ya nyama.
Baada ya kuimarisha kikosi kwa kusajili nyota
kadhaa wapya, kocha Arsene Wenger ataiongoza
Arsenal katika mchezo wa ugenini dhidi ya
Crystal Palace.
Ikiwa imetoka kumaliza ukame wa miaka tisa wa
mataji kwa kushinda Kombe la FA msimu
uliopita, Arsenal ilifungua msimu vizuri kwa
kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifumua
Manchester City 3-0 wiki iliyopita.
Mchezaji mpya, Alexis Sanchez, aliyesajiliwa kwa
Pauni Milioni 30 kutoka Barcelona, anatarajiwa
kuwamo kwenye kikosi cha leo katika mchezo
wa kwanza wa ushindani sambamba na
Nahodha mpya, Mikel Arteta.
Palace inaingia katika mchezo wa leo ikiwa
katika mgogoro, kufuatia taarifa za kuondoka
kwa kocha Tony Pulis juzi baada ya kutofautiana
na wamiliki juu ya sera ya usajili.
Mabingwa wa Championship, Leicester City
watacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu
England tangu mwaka 2004 watakapoikaribisha
Everton leo, wakati timu nyingine iliyopanda
msimu huu, Queens Park Rangers itaikaribisha
Hull City Uwanja wa Loftus Road.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Manchester City
wataanza kutetea taji lao dhidi ya Newcastle
United kesho.
Liverpool, iliyozidiwa kete na Man City katika
mbio za ubingwa msimu uliopita, wataanza
kampeni zao dhidi ya Southampton, ambao
wamewauza Adam Lallana, Rickie Lambert na
Dejan Lovren kwa Wekundu hao wa Anfield.
Lallana ataukosa mchezo huo kutokana na
maumivu ya goti, lakini Lambert na Lovren wote
wapo katika nafasi nzuri ya kuichezea Liverpool,
ambayo imetoka kumuuza kinara wake wa
mabao Luis Suarez kwa Barcelona.
Chelsea ya Mreno Jose Mourinho, ikiongozwa na
wachezaji wake wapya, Diego Costa na Cesc
Fabregas itaifuata Burnley iliyoapanda msomu
huu Jumatatu.
Mechi nyingine; Stoke City na Aston Villa, West
Bromwich Albion na Sunderland na West Ham
United dhidi ya Tottenham Hotspur, wakati kesho
Liverpool v Southampton, Newcastle United v
Manchester City na keshokutwa Burnley

Wednesday, 13 August 2014

VIDAL ANAYEWATOA UDENDA MAN UNITED AONYESHA ISHARA YA KUTUA OLD TRAFFORD

Utata: Kiungo wa Juventus, Arturo Vidal akisaini jezi ya shabiki wa Manchester United 
 KIUNGO Arturo Vidal anayetakiwa na Manchester United ameonyesha ishara fulani, baada ya kusaini jezi ya shabiki wa Mashetani hao Wekundu akiwa kwenye ziara na klabu yake, Juventus nchini Australia.

Monday, 11 August 2014

BBC yazindua ofisi mpya Dar es Salaam


Wafanyakazi wa BBC wakiwa kazini kupeperusha matangazo ya Dira ya Dunia redio
Idhaa ya kiswahili ya BBC imezindua rasmi studio zake mjini Dar es Salaam kwa mbwembwe na haiba kuu.

KOCHA BORA PATRICK PHIRI AJA DAR IJUMAA KUMWAGA WINO SIMBA SC KUREJESHA ENZI ZA MAFANIKIO MSIMBAZI


 
KOCHA bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, Patrick Phiri anatarajiwa kutua Dar es Salaam Ijumaa wiki hii kwa ajili ya kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake ya zamani, Simba SC. Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi. Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

Sunday, 10 August 2014

Ndege nyingine yaanguka na kuua abiria wote

q
Ndege  ya kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makazi ya watu baada kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Magharibi mwa mji wa Tehran nchini Iran.

PATI LA USHINDI NGAO YA JAMII THE GUNNERS LEO...JONEE VITU HAPA

Taji la mapema: Wachezaji wa Arsenal wakifurahia Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Manchester City 3-0 Uwanja wa Wembley, London jioni ya leo

KAULI YA RAIS EVAVS AVEVA WA SIMBA KUHUSIANA NA KUTIMULIWA KWA LOGA HII HAPA


RAIS WA SIMBA, EVANS ELIEZA AVEVA (KUSHOTO) AKITANGAZA UAMUZI WA KUMFUTA KAZI KOCHA ZDRAVKO LOGARUSIC. KULIA NI MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA KLABU HIYO, SAID TULLY. CHINI SOMA BARUA YA AVEVA KUHUSIANA NA KUTIMULIWA KWA LOGA.

MAAJABU YA DUNIA,,JIONEE HUYU SAMAKI AMBAYE YUPO KAMA MTU..


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjYaVlyGuaBVGdvToxoN3D4838pbTJ9N0rRhQOc28AO9nuUXY-suNwe9nGk-Kfwsqmmqok8fq3guWaJE_Bi39Zj5aRSo08EM6qrrz5qJyhKOXiskCrKMOHxpN5BqAOagGC2PdS5gUw_8cAH/s1600/nguva.jpg Habari zilizotufikia Samaki mtu ama nguva ambaye ni adimu sana kuonekana duniani ,,ameonekana amekufa pembezoni mwa bahari nchini ujeruman

Hili ndilo bata refu la Serengeti Fiesta Mwanza lilivyokuwa.jionee picha hapa

Kwa mara ya kwanza Fiesta mwaka 2014 imezinduliwa jijini Mwanza na hii ni baada ya miaka 10 tangu kuzinduliwa msimu huu ambao ilikuwa ni mwak 2004 na ilikua na slogan ya Utamaduni unaendelea.

MAGWIJI WA MAN UNITED NA BAYERN MUNICH WATOSHANA NGUVU JANA ALLIANZ ARENA..JIONEE HAPA

Mido la ukweli: Kiugo wa zamani wa kimataifa wa England, Paul Scholes akimtoka gwiji wa Bayern Munich wakati magwiji wa Manchester United walipomenyana nap katika mechi maalum ya hisani Uwanja wa Allianz Arena jana, wakongwe hao wakitoka sare ya 3-3. 

Haya ndiyo mavazi wanayovaa wahudumu wa ndege kujikinga na Ebola



3Ugonjwa wa Ebola umelipuka sana huko Africa magharibi na umeua watu wengi sana. Hivi sasa mambo mengi yanafanywa ili kukinga watu dhidi ya maambuzi mampya.

Saturday, 9 August 2014

ARSENAL WAIFANYIA 'KISOROKWINYO' MAN UNITED, WAMUUZA VERMAELEN KWA BEI YA UBUYU BARCELONA

Rasmi: Thomas Vermaelen ametua Barcelona baada ya Asrenal kugoma kuwauzia silaha Man United
 NAHODHA wa Arsenal, Thomas Vermaelen amejiunga na Barcelona kwa dau la Pauni Milioni 15 baada ya timu hiyo ya Kaskazini mwa London kugoma kuwauzia silaha wapinzani wa Ligi Kuu England, Manchester United.

EXCLUSIVE# DIAMOND PLATNUMZ LIVE AKIMLA DEN* WEMA NDANI YA ROCK CITY MWANZA...CHEKI HAPA

Yeah Huyo Ni Diamond Platnumz a.k.a Dangote Akifanya Yake Na Madame Wema Sepetu... Love Is In The Air

SIMBA SC YAPIGWA 3-0 NA KIONGERA WAO SIMBA DAY

Mshambuliaji Paul Kiongera wa Simba (kulia), akijaribu kumtoka Simon Silwimba wa Zesco ya Zambia, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa, uliochezwa leo katika sherehe za Simba Day, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-0. 

DANNY MRWANDA ANA GARI AMBALO MCHEZAJI YEYOTE BONGO HANA, WANATUMIA VIGOGO NCHI HII

Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Danny Mrwanda akiwa ameegemea gari lake aina ya BMW X3 lenye thamani ya dola za Kimarekani 85,000 zaidi ya Sh. Milioni 130 za Tanzania. Mrwanda kwa sasa anacheza soka ya kulipwa Vietnam na yuko nchini kwa mapumziko kabla ya kurejea kazini Januari na amepanga kuichezea Polisi ya Morogoro katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

TETESI ZA SOKA ULAYA

Salim Kikeke's photo.

Manchester United wametoa dau la pauni milioni 55 kumtaka kiungo wa Real Madrid Angel Di Maria, 26 (Daily Express), United pia watatazama kumchukua kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, kutoka Barcelona iwapo watashindwa kumpata Arturo Vidal, 27 (Daily Express), Borussia Dortmund wamesema watafanya kila wawezalo kubaki na kiungo wao Marco Reus, 25, licha ya mchezaji huyo kuwindwa na

Friday, 8 August 2014

VIFAA VYA SENEGAL, BOTSWANA VYATUA SIMBA SC

UONGOZI wa klabu ya Simba imenasa vifaa kutoka Botswana na Senegal ambapo watawapima kusaka mchezaji mmoja atakayeziba nafasi moja ya mchezaji wa Kimataifa iliyobaki wazi.
Simba imebakisha nafasi moja kukamilisha usajili wa wachezaji wa Kimataifa ambapo hadi sasa imeishasajili wachezaji Amis Tambwe, Joseph Owino, Kwizera Pierre na Modo Kiongore.
Viongozi wa Simba SC wamepania kutengeneza kikosi kikali kuelekea msimu ujao

GIGSS AIFUNGIA MAN UNITED YA WAKONGWE IKICHAPWA 5-1 NA KITIMU CHA DARAJA LA KWANZA

MKONGWE Ryan Giggs alimtamanisha kocha wake Louis van Gaal baada ya kufunga bao moja magwiji wa Manchester wakifungwa 5-1 na Salford City, timu ambayo kwa sasa anaimiliki kwa pamoja na Paul Scholes, Nicky Butt na Gary na Phil Neville katika mchezo wa hisani uliovutia mashabiki 12,000 Uwanja wa AJ Bell mjini Eccles.

Ukweli kuusu Anti Ezekiel kutoka na dansa wa Diamond Platnumz.

anti ezekielMwanzoni mwa wiki hii miongoni mwa stori ambazo zilitoka na kuenea kwenye magazeti kadhaa ni pamoja na inayomhusu Anti Ezekiel kusemekana kuwa anatoka na dansa wa Diamond Platnumz.

‘Bunge la Katiba lisitishwe’


Mkurgenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba akizungumza na waandishi wa  habari kuhusu mwenendo wa Bunge la Katiba, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mpiganiaji wa Haki za Binadamu, Ananilea Nkya. Picha na Rafael Lubava 

Dar es Salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetaka Bunge Maalumu la Katiba kusitishwa mpaka pale maridhiano baina ya wajumbe yatakapopatikana vinginevyo Katiba itakayopatikana itakosa uhalali wa kisheria na kisiasa.

UN yalaani mateso ya Wakristo Iraq


Mapambano Iraq
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa Jihad wa Iraq dhidi ya wakristo wa eneo wanalolishikilia.
Hii ni baada ya kikao cha dharura cha baraza hilo ambalo lilikutana kujadili hali mbaya ya maeneo ya wakristo, baada ya wapigani wa Jihad kushikilia eneo walilokuwa wakilikalia.

Thursday, 7 August 2014

DIAMOND PLATINUM KUTUMBUIZA SIMBA DAY

SUPASTAA wa wimbo wa My Number One, Nasibu Abduli ‘Diamond’ anatarajia kutumbuiza katika tamasha la Simba Day litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Diamond ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Mdogo Mdogo ataungana na bendi ya Twanga Pepeta kutumbuiza katika tamasha hilo.

Wednesday, 6 August 2014

Manchester United finally convince Vidal to join them at Old Trafford


Manchester United have finally reached a verbal agreement to sign Arturo Vidal according to El Mecurcio. There has been plenty of activity around the potential move with reports now suggesting a £48m and £200k a week deal is on the table in the Express and elsewhere.

MAN UNITED NA BAYERN MUNICH ZA MAGWIJI KUKUMBUSHIA FAINALI LA LIGI YA MABINGWA 1999

Mido kisheti: Paul Scholes ni miongoni mwa wachezaji wa Manchester United wa zamani watakaocheza dhidi ya magwiji wa Bayern Munich katika mechi ya hisani Uwanja wa Allianz Arena Agosti 9
 MAGWIJI wa Manchester United, Paul Scholes, Bryan Robson ana Edwin van der Sar ni baadhi ya wachezaji wa zamani wa Mashetani hao Wekundu watakaocheza mechi ya hisani dhidi ya nyota wenzao wa kitambo wa Bayern Munich Jumamosi.

Francois Nguema:Rais katili aliyeabudu uchawi-2

Joseph Kapinga  

Francois Macias Nguema, alikuwa rais wa kwanza wa Guinea ya Ikweta kuanzia Oktoba 12, hadi Agosti 3, 1979. Nguema anakumbukwa kwa mengi katika utawala wake, lakini kubwa ni tabia yake ya kuamini ushirikina.

Linex nae kaweka nia ya kugombea ubunge,kwa kupitia chama hiki.

mjeda 
Baadhi ya Mastar wa Tanzania wameamua kuweka wazi nia zao za kugombea nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali,miongoni mwa watu hao kwa sasa ni msanii kutoka Kigoma All Stars anaitwa Linex Mjeda.

KARIM BENZEMA SASA 'KUZEEKEA' REAL MADRID

Anabaki Bernabeu: Karim Benzema akiwa ameshika jezi yake namba tisa baada ya kuongeza mkataba Real Madrid 
 MSHAMBULIAJI wa kimataifa nwa Ufaransa, Karim Benzema ameongeza mkataba wa kuendelea kuichezea Real Madrid hadi mwaka 2019 baada ya kukataa kuhamia timu za Ligi Kuu ya England.

HOWARD WEB ATUNGIKA KIPYENGA, SASA BOSI WA MAREFA


Ametungika kipyenga: Howard Webb amehitimisha maisha yake ya urefa 

REFA maarufu England, Howard Webb amestaafu kupuliza kipyenga baada ya miaka 25-na sasa atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya marefa (PGMOL).
Refa huyo mwenye heshima kubwa amechezesha mechi zaidi ya 500 za Ligi Kuu ya England na nyingine za mashindano ya soika nchini humo tangu apande daraja mwaka 2003.

Msichana aliyepigwa na mtoto wa Obama atoa kauli ya kushangaza

 Mtoto wa rais wa kike wa Marekani, Malia Obama mwenye umri wa miaka 16 alimpiga/alimgonga kwa bahati mbaya msichana aliyefahamika kwa jina la Bridget Truskey walipokuwa katika tamasha kubwa la muziki la Lollapalooza nchini Marekani.

Warioba: Bunge litapoteza fedha za wananchi endapo hakuna maridhiano


Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo baada ya kuanza kwa vikao vyake mjini Dodoma jana. 

Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema kuendelea vikao vya Bunge Maalumu la Katiba bila kuwapo maridhiano baina ya pande zinazovutana na upande mmoja ukibaki nje ya Bunge, ni sawa na kutumia vibaya fedha za Watanzania.

Tuesday, 5 August 2014

SAGNA APEWA JEZI NAMBA TATU NA KUANZA RASMI KAZI MAN CITY, NASRI AMFURAHIA ILE MBAYA


Karibu sana: Beki Bacary Sagna kutoka Arsenal akiwa ameshika jezi namba tatu aliyokabidhiwa katika timu yake mpya, Manchester City baada ya kujiunga nayo tasmi jana na kuanza mazoezi Uwanja wa Etihad mjini Manchester.

UKWELI KUHUSU KUACHANA NUH MZIWANDA NA SHILOLE HUU HAPA.


Nuh-MziwandaStori ya Nuh Mziwanda kujichora tatoo yenye jina la Shilole ilisambaa sana na wengi walikua wakijiuliza siku ikitokea wameachana itakuaje hasa upande wa Nuh ambaye ndiye aliyejichora tatoo hiyo.

HIVI NDIVYO MAN UNITED WALIVOPOKELEWA KIFALME WAKITOKEA MAREKANI ..JIONEE HAPA


Wamewasili: Kocha Mholanzi wa Manchester United akiwasili na kikosi chake mjini Manchester wakitokea Marekani ambako walitwaa Kombe la Kimataifa, michuano maalum iliyoandaliwa kwa klabu kujiandaa na msimu mpya

Ali Kiba: Lulu anafaa kuwa mke, aeleza kilichotokea siku ya kifo cha Kanumba

Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo, Wikienda liko bize kukujuza.
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya miaka 18! 

Diamond Vs Ali Kiba : Nay wa Mitego atamani kutembeza kipigo kikali kukomesha


Ushindani kati ya Diamond na Ali Kiba ambao siku zote mimi nauita ‘ushindani usio rasmi’ huku wengine wakiutafsiri kama ‘beef’ umetengeneza mitazamo tofauti kati ya wadau wa muziki Tanzania.

Ukweli kuhusu wimbo wa Linex: Zitto Kabwe ashiriki kukamilisha lyrics 70%, Adam Juma alipwa pesa ambayo hajawahi kulipwa na msanii yoyote, speech yake yaskika wishoni

Wimbo mpya wa Sunday Mjeda a.k.a Linex unaoitwa Wema kwa Ubaya unaotarajiwa kutoka hivi karibuni pamoja na video yake umetengenezwa na producers watatu akiwemo More Fire ambae alisimamia uingizwaji wa vocals, producer Mona Gangstar ambae yeye alishughulikia mixing na kumaliziwa kwa producer Tuddy  Thomas ambae amefanya mastering. 

BREAKING NEWS; YANGA SC YAENGULIWA KOMBE LA KAGAME, AZAM WACHUKUA NAFASI KIGALI


BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiengua Yanga SC katika michuano ya Kombe la Kagame na nafasi hiyo kupewa Azam FC, zote za Tanzania.
Yanga SC imeenguliwa kwa sababu moja tu kubwa, kushindwa kuthibitisha kupeleka kikosi cha kwanza pamoja na kocha Mkuu, Marcio Maximo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.

Monday, 4 August 2014

Picha mpya ya mtoto wa Kanye West na Kim Kardasian yavutia watu mtandaoni.

1
Kim Kardashian alimpereka mtoto North West kwenda kumuangalia baba ake akiwa kazini kwenye studio ya kutengenezea music.