![391755_heroa](http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/05/391755_heroa.jpg)
Bosi wa Barca, Gerardo Martino
Tata ameshindwa kuwatumia wawili hao kama ilivyotarajiwa kutokana na
kukumbwa na majeruhi ya mara kwa mara msimu huu.
Kumekuwepo na taarifa kwenye
vyombo vya habari kuwa wawili hao hawana mahusiano mazuri na hawataki
hata kuonana ana kwa ana, lakini Neymar amesisitiza kuwa yeye na Messi
ni marafiki wakubwa ndani na nje ya uwanja.
“Hatuchezi wote kila mchezo,
lakini nadhani tumejenga uhusiano mzuri tena wakustaajabisha”. Nyota
huyo wa kimataifa wa Brazil amesema wakati wa mahojiano na CNN.
“Watu wengine walisema tusingeelewana, lakini ulikuwa uongo. Ni mtu rafiki sana, ni nyota ninayempenda”.
Neymar alicheza katika fainali ya
Copa del Rey aprili 16 mwaka huu ambapo Barcelona walicharazwa mabao
2-1 na Real Madrid , lakini alipata majeruhi na ilithibitishwa kuwa
atacheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini
kwake Brazil.
Neymar aliongeza: “Nitakuwa fiti
kwa fainali za kombe la dunia. Tatizo pekee ni kwamba siwezi kuisaidia
Barcelona. Natarajia kubeba kombe la dunia na nitawasaidia wenzangu
kutimiza malengo haya”.
“Najua wajibu wangu kwa timu
yangu ya taifa, kama ilivyo kwa wenzangu. Tumekuwa wamoja na
tutasaidiana sana, tunajiandaa kutwaa taji la kombe la dunia”.
Mbrazil huyo pia ametumia nafasi
hiyo kueleza masikitiko yake juu ya utata wa uhamisho wake uliofanyika
mwezi juni mwaka jana kutoka klabu yake ya zamani ya Santos kujiunga na
Barca.
“Kila kitu kilikuwa sahihi na hatukufanya makosa hata kidogo”. Neymar aliendelea.
“Jinsi ambavyo Santos walilichukulia suala langu waliniacha katika huzuni, lakini nitafanya nini”
“Siwezi kuwajibia, lakini
nazungumza kivyangu na kwa ajili ya baba yangu kwamba hatua walizotaka
kuchukua kutatua tatizo hili hazikupendeza”.
No comments:
Post a Comment