MWANAMUZIKI mwenye sauti ya mvuto, Ray C, amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam akikabiliwa na homa kali.
Kwa
mujibu wa vyanzo vyetu, mwanamuziki huyo ambaye amekuwa katika tiba ya
kuachana na matumizi ya dawa za kulevya hospitalini hapo, alifikishwa
hapo jana Jumatatu asubuhi na baadhi ya madaktari walibainisha kuwa Ray C
anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue ambao umelipuka katika maeneo mengi
jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
“Tumemfanyia
vipimo, ana homa kali sana lakini hana malaria. Baada ya kuchunguza
dalili, tumechukua vipimo na kubaini kwamba amepata maambukizi ya
dengue, hivyo tunaendelea kumpa matibabu kwa sasa,” alieleza daktari ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Mwanaspoti
iliyofika wodini alimolazwa mwanamuziki huyo, lilijaribu kuzungumza
naye, lakini manesi wazuia wa kusema hapaswi kuamshwa kwa kuwa alikuwa
amepewa dawa za kutuliza maumivu na kushusha homa.
Ray
C amekuwa katika tiba ya kuacha dawa za kulevya na amekuwa akisaidiwa
kurejea katika sanaa ya muziki ambayo alikuwa akiifanya vizuri kabla ya
kuingia kwenye wimbi hilo.
Ugonjwa
huo dengue uliotajwa kumsumbua kwa sasa umewakumba wananchi wengi wa
Dar es Salaam na unaenezwa na mbu weusi waitwao Aedes Egypitia.
Mbu hao ambao huonekana zaidi mchana, huzaliana katika maji safi yaliyotuama.
Usiku
wa kuamkia juzi Jumapili, Ray C alikuwapo kwenye ukumbi Mlimani City
kwenye hafla ya Tuzo za Muziki za Kilimanjaro ambapo hakuonekana kuwa na
dalili zozote za kuumwa.
No comments:
Post a Comment