Saturday, 10 May 2014

SOKOINE WAMESTAHILI KUPEWA TAIFA STARS, MALINZI WAPATIE NYASI BANDIA

DSC00173Hivi ndivyo watu wa mipango walivyoanza zoezi la uboreshaji wa uwanja wa Sokoine


UWANJA wa kumbukumbu ya Sokoine uliopo jijini Mbeya ni moja ya viwanja vikongwe nchini Tanzania, lakini kwasasa umeanza kurudi katika ubora wake kutokana na marekebisho makubwa yanayofanyika. Meneja wa uwanja huo, Modestus Mbande Mwaluka siku zote anasisitiza kuwa wamiliki wa uwanja huo, CCM kwa kushirikiana na wadau wa soka wanahakikisha wanaukarabati mpaka kufikia hadhi ya kimataifa.

Lengo la watu wa Mbeya ni kuona uwanja huo unatumika katika mashindano makubwa ya kimataifa, hasa kama Mbeya City fc au Prisons watafuzu michuano ya Afrika mwakani. Kwa miaka mingi viwanja vya Uhuru, Taifa na CCM Kirumba vimekuwa vikitumika katika mechi za kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu ya Taifa. Japokuwa uwanja wa Uhuru bado upo katika matengenezo, lakini kabla ya kujengwa kwa uwanja wa kisasa wa Taifa, ulikuwa unatumika zaidi kwa mechi za kimataifa. Uwanja wa CCM Kirumba mara nyingi unatumika kama mbadala wa viwanja vya Dar es salaam. Pia Shk. Amri Abeid ni uwanja ulikuwa unatumika katika mechi za kimataifa miaka ya nyuma kabla ya kudoda. Kwa maana hiyo, mpira wa Tanzania kwa ngazi ya kimataifa ulikuwa anaonwa zaidi katika viwanja hivyo, lakini Dar es salaam ndio kitovu cha soka la Tanzania. Kwasasa kumekuwa na mabadiliko hasa baada ya kuiona Taifa stars ikicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Malawi mei 4 mwaka huu kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment