ZAIDI YA DALADALA 1800 AZITARUHUSIWA KUFANYA SAFARI DAR ES SALAAM BAADA YA MABASI HAYA YAENDAYO KASI KUANZA KAZI
Unaambiwa
Zaidi ya daladala 1,800 hazitoruhusiswa kufanya safari zake maeneo ya
katikati ya jiji la Dar baada ya miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo
haraka kukamilika na ujenzi huo wa miundombinu hiyo inatarajiwa
kukamilika mwisho wa mwaka huu ambapo mabasi 10 madogo na makubwa 20
yatatoa huduma za awali kama majaribio.
Meneja wa uendashaji wa Dart Peter Mnuo amesema Huduma hii ya
majaribio inategemewa kutolewa December mwaka huu na huduma kamili
itaanza kutolewa kuanzia July 2015,wakala wa mabasi hayo yaendayo haraka
umekwishaanza maandalizi ya kutoa huduma ya awali ya mabasi makubwa
kuanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni ikiwa kama sehemu ya mfumo wa kuanza
kutoa huduma.
Mabasi
hayo ya majaribio yanaweza kubeba jumla ya abiria 140 hadi 160 mpaka
hapo itakapoanza kutoka huduma kamili July 2015,mradi huu umepangwa
kutekelezwa kwa awamu 6 ambapo kwa awamu ya kwanza unahudumiwa na fedha
kutoka Bank ya dunia ambapo wao watatoa dolar za kimarekani 290.
No comments:
Post a Comment