Baada ya kuhairishwa kwa Bunge la maalum la
Katiba,Bunge la bajeti linaanza leo Mei 06
Dodoma ambapo wabunge wanatarajiwa
kuanza kulipwa viwango vipya vya posho
ambapo itakua ni shilingi 300,000 kwa siku
ambayo ni sawa na viwango sawa na
walivyokuwa wakilipwa wajumbe bunge
maalum la katiba.
Kabla ya kupandishwa kwa posho hizo
Wabunge walikua wakilipwa 200,000 kwa siku
ambayo mgawanyo wake ulikua ni sawa na
70,000 kama posho ya kikao 80,000 posho ya
kujikimu na 50,000 gharama za usafiri ambapo
nyongeza hiyo ya kila mbunge ambayo ni sawa
na asimilia 50 itaigharimu serikali Tsh Bilioni
18.5 kwa siku 52 zilizotengwa kwa ajili ya
bunge hilo la bajeti.
January 2012 Rais Jakaya Kikwete alikataa
maombi ya bunge ya kutaka nyongeza ya
posho ipande hadi laki tatu na thelathini na
badala yake Wabunge hao wakapata nyongeza
ya elfu 50 tu kwa ajili ya usafiri.
Bunge hili linategemea kumalizika June 27.
Tuesday, 6 May 2014
BUNGE LA POSHO LIMEANZA LEO..NA HIZI NDIZO POSHO WATAKAZOLIPWA ...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment