Profesa J amesema Diamond Platnumz, alilia machozi wakati anafanya chorus ya wimbo wake ‘Kipi Sijasikia’
Rapper huyo alikiambia kipindi cha
Sunrise cha Times FM kuwa wakati Diamond anarekodi chorus hiyo yeye na
Majani walishangaa kumuona hitmaker huyo wa ‘My Number One’ akibubijikwa
na machozi ndani ya ‘booth’.
“Lakini kilichotushangaza alipoingia
booth ili arekodi chorus Diamond alikuwa anaimba huku analia. Sisi tuko
kwenye monitors huku tunamuangalia jamaa upande wa pili kwenye booth
tunamuona Diamond analia.
"Alikuwa emotional unajua ile…ilimgusa
sana. Sisi tulikuwa tunashangaa mimi na Majani ‘huyu jamaa analia nini?’
Lakini baadae tulimuuliza alituambia ‘nimefurahi sana katika maisha
yangu kufanya kazi na Profesa Jay pamoja na Majani, hilo moja.
"Lakini pili, mlivyoimba humu ndani
vyote vinanihusu mimi…vimenitokea sana katika maisha yangu na changamoto
zote hizo’..so yale ndio yalitokea studio. Kiukweli hii ngoma ilikuwa
blessed tangu studio na kila mtu alikuwa anasema ‘yeah men it’s on’,
alisema Profesa J.
No comments:
Post a Comment