KOCHA
wa timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson amesema wachezaji wa
Manchester United wapo hatarini kutojumuishwa katika kikosi chake
kinachotarajia kwenda Brazil kushiriki kombe la dunia kuanzia juni 12
hadi juli 13 mwaka huu.
Bosi huyo wa Simba watatu ameonya
kuwa wachezaji Michael Carrick, Danny Welbeck, Phil Jones, Chris
Smalling, Ashley Young na Tom Cleverley wanaweza kutupwa nje ya kikosi
chake kwasababu ya kiwango kibovu cha klabu yao msimu huu.
Welbeck na Carrick – kwa pamoja
walifanya kazi nzuri wakati wa kampeni za kufuzu fainali za kombe la
dunia, lakini kiwango kibovu cha klabu yao kitaathiri nafasi yao.
Hodgson amesema atachukua
wachezaji wa kikosi chake kwa kuangalia kiwango cha klabu zao, hivyo
amesema timu kama Manchester United wachezaji wake wanaweza kukosa
nafasi.
“Manchester United ni moja ya
klabu chache zenye wachezaji wengi timu ya taifa, lakini wachezaji
lazima wakubali bahati mbaya katika soka lao la England”. Amewaambia The Independence.
“Kama klabu yao inafanya vibaya
maana yake na wao hawafanyi vizuri. Kuna wachezaji wengi wanaofanya
vizuri katika klabu zao, kwahiyo inawatishia nafasi yao katika kikosi
cha timu ya taifa”.
“Nina uhakika wachezaji wa
Manchester United watanielewa kuwa hawana nafasi nzuri ya kucheza timu
ya taifa kwa sasa, kwasababu kiwango chao sio kizuri”.
“Ni wajibu wangu kuchagua wachezaji wenye viwango bora kwa kazi tuliyonayo mbele yetu”
Wayne Rooney hayuko fiti sana,
kwahiyo nafasi yake ya kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Italia ipo
kutegemeana na atakavyoimarika.
Carrick, Welbeck, Jones and
Smalling bado wana uhakika kidogo kuitwa, lakini Cleverley na Young wapo
katika hatari ya kukosa kabisa.
Hodgson atataja kikosi chake mei 12 mwaka huu baada ya kumalizika kwa ligi kuu soka nchini England
No comments:
Post a Comment