Frank Domayo akisaini Azam FC jana |
Viongozi wa Azam FC jana walikwenda kwenye kambi ya Taifa Stars kukamilisha taratibu za usajili na kiungo Frank Domayo, aliyemaliza Mkataba wake Yanga SC.
Baada ya kufanikiwa kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, wasimamizi wa kambi waliwaitia Polisi viongozi wa Azam FC ambao hata hivyo baadaye waliachiwa. Lakini inadaiwa fomu za usajili zilichanwa.
Azam si klabu ya kwanza kusajili mchezaji katika kambi ya timu ya taifa, kwani vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga ndiyo waasisi wa mchezo huo.
Mwaka jana Simba SC walisaini Mkataba mpya na kiungo wao, Amri Kiemba akiwa katika kambi ya Taifa Stars, hoteli ya Tansoma mjini Dar es Salaam.
Inaruhusiwa kwa wakubwa tu; Kiongozi wa Yanga SC, Seif Ahmed 'Magari' alimtoa kambi ya Taifa Stars, beki Kevin Yondan akiwa Simba SC na kumsainisha mwaka 2012. |
Yanga SC iliwasajili Domayo kutoka JKT Ruvu, Kevin Yondan kutoka Simba SC wote wakiwa katika kambi ya Taifa Stars Dar es Salaam miaka miwili iliyopita.
No comments:
Post a Comment